Matamshi ya Scholz yamekuja kwenye mahojiano na televisheni ya CNN Jumapili, siku mbili baada ya kukutana na rais wa Marekani Joe Biden mjini Washington DC. Mafisa wa Marekani katika siku za karibuni wameonya kuwa huenda China ikaanza kutoa misaada ya silaha kwa Moscow.
Kabla ya ziara yake ya Marekani, Scholz aliomba Beijing kujiepusha kutuma silaha kwa Russia na badala yake itumie ushawishi wake kurai taifa hilo kuondoa vikosi vyake nchini Ukraine. Baada ya kuulizwa na CNN iwapo China ingewekewa vikwazo kutokana na kutoa misaada kwa Russia, Scholz alijibu kwamba hilo lingekuwa na matokeo yake, bila kuweka bayana hatua ambayo ingechukuliwa.
Ujerumani ambayo ni uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya pia ndiyo mshirika mkuu zaidi wa kibiashara wa China.