Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:19

Austin: Russia iwapo itafanikiwa kuchukua udhibiti wa Bakhmut, haitawakilisha mabadiliko makubwa vita vya Ukraine


Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amesema Jumatatu ikiwa wanajeshi wa Russia watafanikiwa kuchukua udhibiti wa mji wa mashariki mwa Ukraine wa Bakhmut, hilo halitawakilisha mabadiliko makubwa katika mzozo huo.

"Nadhani hiyo itakuwa ni kama thamani ya mfano kuliko ilivyo thamani ya kimkakati na kiutendaji," Austin aliwaambia waandishi wa habari wakati wa ziara yake nchini Jordan.

Bakhmut imekuwa eneo la mapigano makali kwa miezi kadhaa huku Russia ikishinikiza kuchukua udhibiti wa eneo hilo katika mkoa wa Donetsk nchini Ukraine.

Austin amesema Jumatatu kuwa hatoi tathmini ya uamuzi wa Ukraine wa kuwarejesha wanajeshi wake magharibi mwa mji huo kama pigo la kimkakati kwa Ukraine.

Pia Jumatatu, jeshi la Ukraine liliripoti nzunguko mpya wa mashambulizi ya Russia ikitumia ndege zisizotumia rubani (drone) zilizotengenezwa na Iran.Wizara ya ulinzi ya Ukraine ili-tweet kwamba vikosi vyake vilitungua drone 13 kati ya 15.

Russia imekuwa ikitumia droni za Shahed kushambulia maeneo mbalimbali ya Ukraine, ikiwemo maeneo ya miundombinu.

Wakati huo huo, Russia imesema Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu aliwatembelea wanajeshi wa Russia na kituo cha afya Jumatatu huko kusini mwa Ukraine.

Wizara ya Ulinzi ilisema ziara ya Shoigu huko Mariupol ilihusisha ziara ya mji huo, ambao mwaka jana uliharibiwa na Russia, ili kuangalia juhudi mpya za kuujenga. Wizara hiyo haikufafanua ni wakati gani ziara hiyo ilifanyika.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii inatokana na mashirika ya habari ya AP na Reuters.

XS
SM
MD
LG