Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 16:52

Rais wa Guinea-Bissau avunja bunge bila kutangaza tarehe ya uchaguzi


Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari huko Pretoria Aprili 28, 2022. Picha na Phill Magakoe / AFP.
Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari huko Pretoria Aprili 28, 2022. Picha na Phill Magakoe / AFP.

Rais wa Guinea-Bissau siku ya Jumatatu alivunja bunge kabla ya uchaguzi mpya kufanyika akisema "jaribio la mapinduzi" limelingiza taifa hilo la Afrika Magharibi katika mgogoro mpya.

Rais Umaro Sissoco Embalo, alitoa amri ya kulivunja bunge lenye idadi kubwa ya wapinzani na kutangaza kuwa tarehe ya uchaguzi wa wabunge "itawekwa kwa wakati muafaka, kulingana na katiba".

Ghasia zilizuka kati ya walinzi wa taifa na kikosi maalum cha walinzi wa rais usiku wa Alhamisi katika mji mkuu Bissau, na kusababisha vifo vya watu wawili.

Rais Embalo, ambaye alikuwa Dubai akihudhuria mkutano wa hali ya hewa wa COP28, alirejea Bissau siku ya Jumamosi na kutangaza kuwa "jaribio la mapinduzi" lilikuwa limemzuia kurejea mapema.

Siku ya Jumatatu, alisema kumekuwa na "hujuma" kati ya walinzi wa taifa na "baadhi ya wanasiasa waliomo ndani ya vyombo vya Serikali".

Akimaanisha "utendaji wa kawaida wa taasisi za serikali umekuwa mgumu".

"Ukweli huu unathibitisha uwepo wa mgogoro mkubwa wa kisiasa," aliongeza.

Walinzi wa taifa walikivamia kituo cha polisi siku ya Alhamisi jioni na kumchukua Waziri wa Fedha Souleiman Seidi na Katibu wa Hazina Antonio Monteiro, ambao walikuwa wakishikiliwa kwa mahojiano, kulingana na maafisa wa jeshi na wa kijasusi.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG