Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 04, 2024 Local time: 12:13

Watawala wa kijeshi Afrika Magharibi waahidi kushirikiana


Jenerali Abdourahamane Tiani, akisoma taarifa kwenye televisheni ya taifa Agosti 19, 2023.
Picha na ORTN - Télé Sahel / AFP
Jenerali Abdourahamane Tiani, akisoma taarifa kwenye televisheni ya taifa Agosti 19, 2023. Picha na ORTN - Télé Sahel / AFP

Mtawala wa kijeshi wa Niger Jenerali Abdourahamane Tiani alikutana na viongozi wenzake wa Mali na Burkina Faso katika ziara yake ya kwanza ya kimataifa tangu kutwaa mamlaka mwezi Julai.

Majirani wa Niger, Mali na Burkina Faso -- ambazo zinatawaliwa na viongozi wa kijeshi walionyakua mamlaka mwaka 2020 na 2022 mtawalia - wameahidi mshikamano na viongozi wa mapinduzi ya Niger.

Tiani aliwasili Burkina Faso Alhamisi jioni kwa ziara ya kuendeleza uhusiano na Kapteni Ibrahim Traore.
Wawili hao walijadili "maswala ya kawaida kwa nchi zote mbili, haswa mapambano dhidi ya ugaidi na maendeleo ya kijamii na kiuchumi", kulingana na taarifa kutoka kwa rais wa Burkina.

Nchi hizo tatu za Afrika Kaskazini ya Kati mnamo Septemba zilitia saini makubaliano ambayo yanajumuisha ulinzi wa pande zote ikiwa kutatokea tukio la shambulio la "uhuru na uadilifu wa eneo" la nchi yoyote kati ya hizo

Forum

XS
SM
MD
LG