Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 04, 2024 Local time: 12:16

Wanajeshi 60 wa Guinea wasimamishwa kazi kutokana na uvamizi wa jela mwishoni mwa wiki


Maafisa wa usalama wakishika doria karibu na jela anaposhikiliwa Moussa Dadis Camara, mjini Conakry.
Maafisa wa usalama wakishika doria karibu na jela anaposhikiliwa Moussa Dadis Camara, mjini Conakry.

Utawala wa kijeshi wa Guinea umesimamisha kazi wanajeshi 60 pamoja na maafisa wa jela, baada ya watu wenye silaha mwishoni mwa wiki kumtoa jela kiongozi wa zamani wa kijeshi Moussa Dadis Camara, maafisa wa serikali wamesema Jumatatu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, watu waliokuwa wamejihami vikali walivamia jela hiyo iliyopo kwenye mji mkuu wa Conakry, na kumtoa Camara pamoja na maafisa wengine watatu waliokuwa wakikabiliwa na mashitaka ya mauaji ya halaiki ya 2009, alipokuwa rais wa taifa hilo.

Haijabainika iwapo watu hao walitoroka jela au walichukuliwa kinyume cha mapenzi yao kulingana na mawakili wao, taarifa zikiongeza tukio hilo linahujumu mageuzi ya serikali, wakati jeshi likiapa utiifu kamili kwa utawala wa uliopo.

Mamlaka zimesisitiza kuwepo kwa utulivu, na kusema kwamba hali ya usalama imedhibitiwa. Kufikia Jumatatu, hali ya kawaida imeripotiwa kurejea kwenye kitongoji cha Conakry cha Kaloum, ambako jela iliyovamiwa inapatikana.

Hali ya usalama hata hivyo imeimarishwa wakati ukaguzi wa magari yanayoingia na kutoka Kaloum yakikaguliwa na maafisa wa usalama. Mawakili wa Camara pamoja na jeshi walitangaza Jumamosi jioni kwamba alikamatwa tena na kurejeshwa kwenye jela, bila kutoa maelezo zaidi. Watu wengine wawili waliotoroka naye wakati wa uvamizi huo pia wamerejeshwa kizuizini.

Guinea yenye idadi ya watu milioni 14 inaongozwa na Kanali Mamady Doumbouya ambaye baada ya kufanya mapinduzi ya kijeshi yaliomuondoa rais aliyechakuliwa na rais, Alpha Konde, Septemba, 2021.

Mamalaka ilipata miili ya washambuliaji watatu , wanajeshi wanne na watu wengine wawili, wizara ilisema katika ripoti yake ya kwanza rasmi, wakati jela ilipovunjwa.W engine sita walikuwa hospitali na majeraha ya bunduki , iliongeza taarifa hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG