Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 08:27

Waziri wa kigeni wa Ufaransa aahidi kushirikiana na ECOWAS kurejesha demokrasia Afrika Magharibi


Waziri wa mambo ya masuala ya kigeni na Ulaya wa Ufaransa Catherine Colonna. Picha ya Septemba 18, 2023
Waziri wa mambo ya masuala ya kigeni na Ulaya wa Ufaransa Catherine Colonna. Picha ya Septemba 18, 2023

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa amesema kwamba Ufaransa itashirikiana na Umoja wa Kiuchumi wa Mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS, kwenye harakati zake za kurejesha demokrasia ya kieneo

Hatua hiyo ni baada ya baadhi ya mataifa wanachama kukumbwa na mapinduzi ya kijeshi hivi karibuni, pamoja na hali ya usalama inyoendelea kudorora kwenye mataifa ya Sahel. Waziri Catherine Colonna yupo ziarani Nigeria ambayo ni mwenyekiti wa sasa wa ECOWAS, wakati wakizungumzia ushirikiano wa kimataifa pamoja na usalama wa kikanda.

Ufaransa katika siku za karibuni imesitisha operesheni za kijeshi dhidi ya makundi ya wanajihadi nchini Mali na Burkina Faso, wakati hivi karibuni ikiondoa wanajeshi wake kutoka Niger. Mataifa yote matatu yanaongozwa na maafisa wa kijeshi baada ya kufanyika kwa mapinduzi.

Harakati za mpito kuelekea demokrasia zimekwama Mali na Burkina Faso, wakati utawala wa kijeshi wa Niger ukipuuzia amri ya ECOWAS ya kurejesha mara moja utawala wa kiraia, na badala yake kusisitiza kipindi cha mpito cha miaka 3.

ECOWAS tayari imewekea Niger vikwazo, wakati kukiwa na uwezekano kutumia jeshi katika kutanzua mzozo uliyopo. Wakati akikutana na mwenzake wa Nigeria Yusuf Tugaar mjini Abuja, waziri Colonna amesema kwamba wamezungumzia kuhusu kuunga ECOWAS mkono, kwenye juhudi zake za kurejesha utawala wa kikatiba nchini Mali, Burkina Faso na Niger.

Forum

XS
SM
MD
LG