Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 04, 2024 Local time: 22:47

Watu wenye silaha wawauwa wanafunzi 13 Nigeria


Maafisa wa usalama wakilinda kijiji cha Kukawa katika enei la Kanan Nigeria baada ya nyumba za wakazi kuchomwa na majambazi, Aprili 12, 2022. Picha ya AFP
Maafisa wa usalama wakilinda kijiji cha Kukawa katika enei la Kanan Nigeria baada ya nyumba za wakazi kuchomwa na majambazi, Aprili 12, 2022. Picha ya AFP

Watu wenye silaha kutoka magenge ya uhalifu waliwauwa wanafunzi 13 wa shule ya msingi ya Kiislamu wakati wa hafla ya kusherekea kuzaliwa kwa Mtume Mohammed katika jimbo la kaskazini magharibi la Katsina, afisa wa eneo hilo amesema Jumanne.

Katsina ni moja ya majimbo kadhaa kaskazini magharibi na katikati mwa Nigeria yanayokumbwa na mashambulizi ya magenge ya uhalifu, yanayojulikana kama majambazi, ambao huvamia vijiji, kuua na kuteka nyara wakazi pamoja na kuchoma nyumba zao baada ya kuwapora.

Magenge hayo, ambayo yana ngome katika misitu mikubwa inayozunguka majimbo ya Zamfara, Katsina, Kaduna na Niger, yamekuwa mashuhuri kwa utekaji nyara mkubwa wa wanafunzi wa shule katika miaka ya hivi karibuni.

Watu kadhaa wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki walishambulia kijiji cha Kusa katika wilaya ya Musawa nyakati za usiku siku ya Jumapili na kuwafyatulia risasi watoto wa shule wakisherekea Maulidi katika kijiji hicho, kiongozi wa wilaya ya Musawa Habibu Abdulkadir ameiambia AFP kwa njia ya simu.

Forum

XS
SM
MD
LG