Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 10:48

Wanasheria waitaka mahakama kumrejesha rais wa Niger madarakani


 Rais wa zamani wa Niger aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum
Rais wa zamani wa Niger aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum

Wanasheria wa rais wa Niger aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum ameiomba mahakama ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi siku ya Jumatatu kuamuru kurejeshwa kazini kwa rais huyo, wakidai kuwa kuzuiliwa na kupinduliwa kwake kulikiuka haki zake.

Bazoum amekuwa akishikiliwa tangu wanajeshi wachukue mamlaka terehe 26 Julai, wakimtuhumu Bazoum kwa kushindwa kudhibiti hali ya ukosefu wa usalama nchini humo – ni moja ya mapinduzi nane yaliyofanyika katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita huko Afrika Magharibi na Kati.

Mawakili wake waliwasilisha kesi yake kwenye Mahakama ya Haki ya Jamii, iliyoundwa kushughulikia kesi katika kambi ya kikanda ya ECOWAS - ingawa siyo lazima nchi wanachama wafuate maagizo yake na hakuna mfumo wa kufanya maamuzi yake kuwa ya lazima.

Mmoja katika timu ya wanasheria ya Bazoum, Seydou Diagne, ameitaka mahakama hiyo yenye makao yake katika mji mkuu wa Nigeria Abuja kutoa uamuzi kuwa "kuuondoa kikatili serikali ya Bazoum kumekiuka haki zake za kisiasa." Diagne, akizungumza kupitia kiungo cha video kutoka mji mkuu wa Senegal.

Dakar, ilisema Bazoum inapaswa kuachiliwa huru bila masharti na kurejeshwa kuwa rais.

Mawakili hao pia wamesema kuzuiliwa kwake, mkewe na mwanawe kunakiuka haki zao za kibinadamu.

Wakili wa serikali ya Niger, Aissatou Zada, aliiambia mahakama kwamba Bazoum, mkewe na mwanawe hawakuwekwa kizuizini kiholela au kutengwa. Alisema walikuwa huru kuingia na kuondoka kama wakitaka, lakini rais Bazoum alishikiliwa nyumbani kwa ajili ya usalama wake.

Mawakili wa Bazoum walisema hawajaweza kuzungumza naye tangu Oktoba 20, baada ya jeshi kumshutumu rais huyo wa zamani kwa kujaribu kutoroka kwa msaada wa washirika. Mahakama imepanga kutoa uamuzi kuhusu kesi hiyo Novemba 30.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG