Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 23, 2024 Local time: 02:23

Marekani yakataa muswada wa kuondoa wafanyakazi wake Niger


Baraza la senate la Marekani, Alhamisi limekataa kabisa muswada utakao mlazimisha rais Joe Biden, kuondoa wanajeshi wa Marekani, Niger, taifa la Afrika Masgharibi ambalo jeshi linashikilia madaraka toka Julai.

Mswada huo wa sheria ulipingwa kwa kura 86 dhidi ya 11. Marekani mwezi huu ilitangaza rasmi kwamba kutokana na mapinduzi ya Niger, imesimamisha msaada, lakini maafisa wa Marekani, wamesema hakuna mpango wa kubasilisha uwepo wa wanajeshi wa Marekani, nchini humo.

Niger, imekuwa mshirika wa Wahington, katika kukabiliana na wanamgambo wenye msimamo mkali ambao wameua maelfu ya watu, la kukosesha makazi mamilioni zaidi barani Afrika.

Kuna wafanyakazi wa wizara ya ulinzi 1,000 ndani ya taifa hilo. Seneta wa Republikan, Rand Paul, ambaye aliwasilisha muswada, ametoa hoja kwamba wanajeshi hawakupelekwa kwa kufuata kanuni za Baraka za bunge, na kusema Wamarekani, hawapaswi kuwa hatarini katika mgogoro wa Niger.

Forum

XS
SM
MD
LG