Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 13:51

Ufaransa kuiunga mkono ECOWAS katika kurejesha demokrasia Sahel


Kamati ya Wakuu wa Majeshi ya ECOWAS ilipokutana mjini Accra, Ghana. Agosti 17, 2023. REUTERS/Francis Kokoroko
Kamati ya Wakuu wa Majeshi ya ECOWAS ilipokutana mjini Accra, Ghana. Agosti 17, 2023. REUTERS/Francis Kokoroko

Ufaransa itaiunga mkono zaidi jumuiya ya Afrika Magharibi ECOWAS wakati ikifanya kazi kurejesha demokrasia katika eneo ambalo hivi karibuni limekumbwa na mapinduzi, huku ukosefu wa usalama katika Sahel unazidi kuwa mbaya, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa alisema Ijumaa.

Waziri wa Ulaya na Masuala ya Mambo ya Nje Catherine Colonna alikuwa akiitembelea Nigeria, mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi, kujadili ushirikiano wa nchi mbili na pia usalama wa kikanda.

Ufaransa imemaliza shughuli zake za kijeshi dhidi ya jihadi nchini Mali na Burkina Faso na hivi karibuni ilianza kuondoa vikosi vyake kutoka Niger -- nchi zote tatu ambazo hivi sasa zinatawaliwa na utawala wa kijeshi baada ya mapinduzi.

Kipindi cha mpito kuelekea demokrasia kimekwama nchini Mali na Burkina Faso na utawala wa kijeshi wa Niger pia umepuuza madai ya ECOWAS ya kurejesha mara moja utaratibu wa kikatiba na kusisitiza kuhusu kuwepo kwa serikali ya mpito hadi miaka mitatu.

ECOWAS imeiwekea Niger vikwazo huku ikiacha wazi uwezekano wa kuingilia kijeshi kama chaguo la mwisho ikiwa litahitajika.

Alipokutana na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Nigeria Yusuf Tuggar mjini Abuja, Colonna amesema wamejadiliana kuiunga mkono ECOWAS kurejesha utulivu wa kikatiba nchini Mali, Burkina Faso na Niger.

Viongozi wa kijeshi nchini Niger wameitaka Ufaransa kuwaondoa wanajeshi wake 1,500 ambao wanapanga kuondoka ifikapo mwisho wa mwaka.

Chanzo cha habari hii ni shiika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG