Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 06:15

Serikali ya kijeshi ya Niger yatangaza kuondoa sheria ya kupambana na uhamiaji


Jenerali Abdourahmane Tiani, ambaye alitangazwa kuwa mkuu mpya wa nchi ya Niger na viongozi wa mapinduzi, walipokutana na mawaziri huko Niamey.REUTERS
Jenerali Abdourahmane Tiani, ambaye alitangazwa kuwa mkuu mpya wa nchi ya Niger na viongozi wa mapinduzi, walipokutana na mawaziri huko Niamey.REUTERS

Serikali ya kijeshi ya Niger imetangaza Jumatatu kwamba imeondoa sheria ya kupambana na uhamiaji ambayo ilikuwa imesaidia kupunguza kukimbia kwa watu wa Afrika Magharibi Kwenda Ulaya

Serikali ya kijeshi ya Niger imetangaza Jumatatu kwamba imeondoa sheria ya kupambana na uhamiaji ambayo ilikuwa imesaidia kupunguza kukimbia kwa watu wa Afrika Magharibi Kwenda Ulaya lakini ambayo ilikosolewa vikali na wakazi wa jangwani ambao uchumi wao ulikuwa ukitegemea usafirishaji watu kwa muda mrefu.

Sheria hiyo, ambayo iliharamisha kusafirisha wahamiaji kupitia Niger, ilipitishwa Mei 2015 huku idadi ya watu wanaosafiri kupitia Bahari ya Mediteranian kutoka Afrika ikifikia kiwango cha juu zaidi, na kusababisha mzozo wa kisiasa na kibinadamu huko Ulaya ambapo serikali zilishinikizwa kusitisha usafirishaji.

Wanajeshi wa Niger, ambao walichukua mamlaka katika mapinduzi ya Julai, waliiondoa sheria hiyo siku ya Jumamosi na kuitangaza Jumatatu jioni kwenye televisheni ya taifa.

Utawala huo unatathmini upya uhusiano wake na washirika wake wa zamani wa nchi za magharibi ambao walishutumu mapinduzi hayo, na inatafuta kupata uungwaji mkono nyumbani, ikiwa ni pamoja na jumuiya za kaskazini mwa jangwa ambazo zilifaidika zaidi kutokana na uhamiaji huo.

Forum

XS
SM
MD
LG