Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 04, 2024 Local time: 12:36

Rais wa Sierra Leone atangaza amri ya kutotoka nje


Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura yake katika uchaguzi wa kitaifa katika kituo cha Freetown, Sierra Leone, Juni 24, 2023. REUTERS/Cooper Inveen
Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura yake katika uchaguzi wa kitaifa katika kituo cha Freetown, Sierra Leone, Juni 24, 2023. REUTERS/Cooper Inveen

Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio ametangaza amri ya kutotoka nje kote nchini humo baada ya watu wenye silaha kushambulia kambi kuu ya kijeshi ya taifa hilo

Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio ametangaza amri ya kutotoka nje kote nchini humo baada ya watu wenye silaha kushambulia kambi kuu ya kijeshi ya taifa hilo la Afrika Magharibi katika mji mkuu, na kuzua hofu ya kuvunjika kwa utulivu huku kukiwa na ongezeko la mapinduzi katika eneo hilo.

Bio alisema Jumapili, katika taarifa yake kwenye mtandao wa X, kwamba watu wenye silaha wasiojulikana walishambulia ghala ya silaha katika mji mkuu, Freetown, mapema asubuhi. Aliandika kwamba utulivu umerejeshwa na vikosi vya usalama vinawatafuta watu hao wenye silaha.

Bio alichaguliwa tena kwa muhula wa pili mwezi Juni katika kura iliyopingwa ambapo chama kikuu cha upinzani kiliishutumu tume ya uchaguzi ya Sierra Leone kwa kula njama na chama chake ili kuiba matokeo.

Wakati huo huo mamlaka ya usafiri wa anga ya Sierra Leone siku ya Jumapili iliyataka mashirika ya ndege kuahirisha safari za ndege baada ya amri ya kutotoka nje nchi nzima iliyowekwa na serikali ili kukabiliana na shambulio kwenye kambi ya kijeshi na watu wenye silaha wasiojulikana.

Mamlaka ya usafiri wa anga ilisema katika taarifa kwamba abiria wanapaswa kuwekwa kwenye ndege zinazofuata baada ya amri ya kutotoka nje kuondolewa. Iliongeza kuwa anga ya nchi bado iko wazi.

Forum

XS
SM
MD
LG