Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 07:38

Mapigano yalianza Jumapili kati ya jeshi la Mali na makundi ya wanaotaka kujitenga


Wapiganaji wa Tuareg nchini Mali
Wapiganaji wa Tuareg nchini Mali

Afisa mmoja wa jeshi ameliambia shirika la habari la AFP kwamba jeshi la Mali “limeanzisha tena operesheni zake ardhini ili kulilinda eneo lote la taifa hilo”. Na kwamba “mapigano yameanza tena karibu na Kidal” na wenyeji wanaweza “kusikia sauti za roketi”.

Mapigano yalianza tena Jumapili kati ya jeshi la Mali na makundi ya wanaotaka kujitenga ya Tuareg na waasi katika mkoa wa kaskazini mwa nchi hiyo, maafisa wa jeshi na maafisa waliochaguliwa wamesema.

Tangu jeshi lichukue madaraka kwa njia ya mapinduzi mwaka 2020, watawala hao wa kijeshi katika nchi hiyo ya Afrika wameweka kipaumbele cha kuanzisha upya mamlaka katika mikoa yote na Kidal ambapo inaweza kuwa uwanja mkuu wa mapambano.

Afisa mmoja wa jeshi ameliambia shirika la habari la AFP kwamba jeshi la Mali “limeanzisha tena operesheni zake ardhini ili kulilinda eneo lote la taifa hilo”. Afisa mmoja katika eneo hilo, pia akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina alisema kuwa “mapigano yameanza tena karibu na Kidal” na wenyeji wanaweza “kusikia sauti za roketi”.

Ndege za kijeshi zilionekana zikielekea Kidal leo Jumapili, afisa mwingine alisema. Mapigano yalianza siku moja kabla wakati jeshi lilipolifunga eneo hilo, baada ya kutangaza Alhamisi kwamba lilianza harakati za kimkakati zinazolenga kuimarisha usalama na kutokomeza vitisho vyote vya kigaidi katika mkoa wa Kidal.

Forum

XS
SM
MD
LG