Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:53

Raia wa Afrika Kusini wakerwa na viongozi wao kushindwa kumuenzi Mandela


Hayati Nelson Mandela
Hayati Nelson Mandela

Kila mwaka Julai 18 siku ya kuzaliwa Nelson Mandela, serikali ya Afrika Kusini  inawataka raia wake kuheshimu urithi aliouacha na mazuri mengi aliyofanya.

Lakini takriban miaka 10 baada ya kifo cha mpambanaji maarufu dhidi ubaguzi wa rangi, huku Afrika Kusini ikitaabika kutokana na rekodi ya juu ya ukosefu wa ajira, kuenea kwa kukatika umeme na kashfa ya ufisadi, wengi wanasema serikali iliyoko madarakani yenyewe imefeli kumuenzi Mandela.

Mandela, alikaa gerezani miaka 27 katika mapambano yake dhidi ya utawala wa kibaguzi wa wazungu walio wachache, ni shujaa kwa wengi nchini Afrika Kusini na kote duniani.

Baada ya kuwa rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia mwaka 1994 kulikuwa na hisia kubwa ya matumaini kwa Afrika Kusini chini ya uongozi wake katika Chama cha African National Congress, au ANC.

Lakini warithi wake – wote kutoka ANC – wametathminiwa kimchanganyiko, huku mmoja – Rais wa zamani Jacob Zuma – akikabiliwa na kesi kadhaa za ufisadi.

Wakosoaji wengi wanasema chama cha ukombozi kilichosimuliwa wakati fulani kimekuwa na mengi, ufisadi, na bila stadi, japokuwa wengine wanadai kuwa urithi wa mfumo wa kikatili wa kibaguzi umefanya iwe vigumu kuleta mabadiliko nchini.

Kile Waafrika Kusini wa kawaida waliozungumza na VOA katika mitaa ya Johannesburg walichokubaliana kuhusu siku hii ya Mandela, lakini, hivi huyo ndiyo yule mtu ambaye wengi walikuwa wamuita “tata” au baba, wana majonzi ya kutokuwepo nao.

Isaac Rabotapi, mlinzi, anakumbuka siku moja mwaka 1990 alipokuwa kijana mdogo na Mandela alikuwa ameachiliwa huru kutoka jela.

“Tulikuwa na furaha sana huko Soweto … hata watoto, hatukuweza kulala hata siku hiyo kwa sababu tulikuwa na furaha kubwa kwa kuachiliwa huru… Tunakumbuka vitu vingi sana kuhusu yeye. Kwa kweli tuna majonzi kutokuwa naye.

Rabotapi anasema viongozi wa sasa wa nchi hiyo hawajafanya katika kuuenzi urithi mkuu wa Mandela.

“Nimesikitishwa sana. Nafikiri Tata anagelia kuona kuwa Afrika Kusini inadidimia; kweli, inaporomoka kutokana na kukosekana maji, mgao wa umeme, kukatika kwa umeme, uhaba wa chakula, wewe unajua, vitu vingi. Uhalifu.”

Agnes Mashole, ambaye anamiliki saluni ya urembo, pia anakumbuka sherehe kadhaa wakati Mandela na ANC waliposhinda uchaguzi wa kwanza baada ya ubaguzi wa rangi kumalizika.

Lakini kama Rabotapi, analalamika kuenea kwa ukosefu wa umeme unaojulikana kama “loadshedding” – hali iliyoathiri vibaya uchumi wa uchumi ulioendelea zaidi Afrika –anaeleza masikitiko yake kuhusu serikali iliyoko madarakani.

“Wao walifeli, kwa kweli wameshindwa. Natamani tungeweza kumuamsha Mandela na kurekebisha kila kitu… Uchumi unadidimia. Kuna mgao wa umeme. Hali ni mbaya zaidi.

Asanda Ngoasheng, mchambuzi wa siasa wa kujitegemea, ameiambia VOA Afrika Kusini ilikuwa nchi ngumu kwa sababu ya historia yake.

Sanamu la Rais wa zamani Nelson Mandela na mkewe Winnie Madikizela-Mandela katika eneo la utalii maarufu kama The Long March to Freedom
Sanamu la Rais wa zamani Nelson Mandela na mkewe Winnie Madikizela-Mandela katika eneo la utalii maarufu kama The Long March to Freedom

“Ndio, ufisadi unaacha doa ndani ya ANC na ni suala gumu sana kukabiliana nalo na linawafadhaisha Waafrika Kusini hasa ukizingatia urithi wa Mandela, lakini kuna mengi ambayo ANC imefanya kwa ajili ya Afrika Kusini na inaendelea kufanya kwa ajili ya Afrika Kusini, hususan Watu Weusi wa Afrika Kusini.

Katika kuadhimisha Siku ya Mandela, Rais Cyril Ramaphosa amezindua masanamu mawili mapya ya kiongozi anayeheshimiwa, na akatoa hotuba kuhusu “kufuata mwenendo wake.”

Hata hivyo, iwapo ANC haitarekebisha baadhi ya matatizo yanayoisibu nchi, inawezekana haitoweza kuendelea kushikilia madaraka kwa kutumia heshima ya Mandela.

Afrika Kusini itafanya uchaguzi mwaka ujao na kura za maoni zinaonyesha ANC inaweza kupoteza wingi wake katika bunge kwa mara ya kwanza tangu kuingia madarakani.

Forum

XS
SM
MD
LG