Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 03:02

Mfalme wa Zulu akanusha madai ya kupewa sumu, asema afya yake iko shwari


(FILES) Mfalme wa Zulu, Misuzulu Kazwelithini.
(FILES) Mfalme wa Zulu, Misuzulu Kazwelithini.

Mfalme wa Zulu, mkuu wa ufalme wa kitamaduni wenye ushawishi mkubwa zaidi nchini Afrika Kusini, alisema Jumatatu "alikuwa salama," na akakanusha uvumi kwamba alikuwa amepewa sumu.

Misuzulu Kazwelithini aliliambia shirika la habari la AFP katika mahojiano ya simu kutoka nchi jirani ya Eswatini, ambako anafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu, kwamba hali yake ya afya ni shwari.

Kazwelithini, maarufu kama Zulu, mwenye umri wa miaka 48, alichukua usukani mwaka jana, kufuatia mzozoz mkali kuhusu urithi wa kifalme, baada ya kifo cha babake, Goodwill Zweli-thini.

Mwishoni mwa wiki, waziri mkuu wa Zulu mwenye ushawishi mkubwa, Mwanamfalme Mangosuthu Buthelezi, alisema kuwa mfalme huyo amelazwa hospitalini nchini Eswatini baada ya kuugua.

Buthelezi alisema kulikuwa na "tuhuma kwamba alipewa sumu," baada ya kifo kisichotarajiwa cha mmoja wa washauri wake wa karibu. Mfalme Kazwelithini alikanusha ripoti za kulazwa hospitalini, alipozungumza na AFP.

"Ulikuwa uchunguzi wa kawaida wa utaratibu ambao mimi hufanya kila baada ya miezi mitatu, wakati mwingine kila baada ya miezi sita," alisema katika mahojiano mafupi.

Msemaji wa kifalme, Mwanamfalme Africa Zulu, aliliambia shirka la habari la AFP siku ya Jumatatu kwamba mfalme huyo alitumia siku nzima kufanya kazi, ikiwa ni pamoja na kukutana na wajumbe wa China, lakini hakutoa maelezo zaidi.

Forum

XS
SM
MD
LG