Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:28

Afrika Kusini yatarajiwa kupata mvua zaidi maeneo yaliyopata mafuriko


Athari za mafuriko na mvua kubwa katika eneo la KwaZulu Natal, Afrika Kusini.
Athari za mafuriko na mvua kubwa katika eneo la KwaZulu Natal, Afrika Kusini.

Zaidi ya watu 300 wamefariki katika mafuriko ndani na karibu na mji wa pwani ya mashariki wa Durban katika siku za hivi karibuni.

Afrika Kusini inatarajia kupata mvua kubwa zaidi katika wilaya zilizokumbwa na mvua kubwa na mbaya mapema wiki hii.

Zaidi ya watu 300 wamefariki katika mafuriko ndani na karibu na mji wa pwani ya mashariki wa Durban katika siku za hivi karibuni.

Siku ya Jumatano Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alieleza mafuriko hayo ni janga kubwa akiunganisha moja kwa moja na dharura ya hali ya hewa.

Rais Ramaphosa amesema haya: “ kitu kigumu ni kwamba tumepoteza maisha ya watu wengi na nyumba zao zimeharibiwa na maji , barabara pia zimeharibiwa pamoja na madaraja. Na hapa pia kanisa hili limeharibiwa na maji , nyumba zimebomolewa na hilo limetengeneza tatizo kwa hiyo tunafikiria tuje hapa ili tujionee wenyewe.”

Idara ya hali ya hewa ya Afrika kusini imeonya kuendelea kuwepo upepo mkali na mvua itakayosababisha mafuriko zaidi katika jimbo la kwa Zulu-Natal na baadhi ya majimbo mengine mwishoni mwa wiki wakati wa sikukuu ya Pasaka.

Watabiri wa hali ya hewa wamesema mafuriko yametokea ghafla.

XS
SM
MD
LG