Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:58

Watano wafariki katika mafuriko na maporomoko Afrika Kusini


Mafuriko yaliokumba Afrika kusini.
Mafuriko yaliokumba Afrika kusini.

Takriban watu watano wamefariki dunia katika mafuriko na maporomoko ya matope  katika mji wa bandari wa Durban nchini Afrika Kusini kufuatia mvua kubwa iliyonyesha siku za hivi karibuni, maafisa  wamesema Jumanne.

Siku kadhaa za mvua zimepelekea mafuriko katika maeneo kadhaa na kufunga barabara nyingi katika jiji hilo, ambalo ni maarufu kwa fukwe zake za kupendeza.

Vifo vitano vimeripotiwa kufikia sasa lakini bado tuna kukusanya taarifa kutoka kwa watu wa huduma za dharura," Lungi Mtshali, msemaji wa wizara ya Utawala wa Ushirika, aliiambia AFP.

Kanda za video zilizoshirikishwa na wafanyakazi wa uokoaji wa binafsi na wahudumu wa afya zinaonyesha barabara kuu za jiji hilo zilizofurika, magari yaliyozama na nyumba zilizoanguka.

XS
SM
MD
LG