Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 16:02

Mafuriko yaua watu kadhaa Afrika kusini


Mtu aliyesimama kwenye sehemu ya gari la kubeba mizigo akijiokoa kutokana na mafuriko Ladysmith, KwaZulu Natal, Jan 17 2022. PICHA: AP
Mtu aliyesimama kwenye sehemu ya gari la kubeba mizigo akijiokoa kutokana na mafuriko Ladysmith, KwaZulu Natal, Jan 17 2022. PICHA: AP

Watu 45 wamefariki kutokana na mafuriko katika jimbo la Kwa Zulu Natal, Afrika kusini.

Mvua kubwa iliyonyesha jumatatu, iliharibu nyumba, barabara na kupelekea watu kadhaa kukoseshwa makazi.

Serikali ya jimbo la KwaZulu natal imethibitisha idadi ya watu ambao wamefariki na kusema kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka.

Mvua kubwa inatarajiwa kuendelea kunyesha katika sehemu za pwani za mkoa huo.

Timu ya kushughulikia majanga inaendelea kuwahamisha watu kutoka sehemu ambako maporomoko ya matope yametokea na nyumba zimeanguka.

Nyumba kadhaa zimesombwa na mafuriko hayo huku barabara zikibomoka.

Jeshi la Afrika kusini linaendelea kutoa msaada kwa kutumia helikopta katika sehemu ambazo usafiri umeharibika kabisa baada ya barabara kusombwa na mafuriko hayo.

XS
SM
MD
LG