Alishinda tuzo ya dansi na muziki bora kabisa kutokana na album yake ambayo imewavutia watu wengi.
Black Coffee alisema tuzo yake ni kwa heshima ya waafrika wanaochipukia na kukuza vipaji vyao.
Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa amemshukuru kwa kuwapa motisha kizazi kipya.
Mwimbaji Angélique Kidjo alishinda tuzo ya muziki bora wa mwaka kutokana na album yake inayohusu mazingira, ambayo aliwashirikisha wanamuziki wa Nigeria Burna Boy, Yemi Alade na Mr Eazi.
Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 61, aliwashinda Wizkid, Femi Kuti wa Nigeria, na Rocky Dawuni wa Ghana kwa tuzo hiyo, ambayo ni yake ya tano ya Grammy.