Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 12:24

Kampeni ya polio yazinduliwa katika nchi nne barani Afrika

Kampeni ya chanjo inaendelea Malawi.
Kampeni ya chanjo inaendelea Malawi.

Kampeni ya kuwachanja watoto zaidi ya milioni 9 dhidi ugonjwa wa polio imezinduliwa wiki hii katika nchi nne za kusini na mashariki mwa Afrika baada ya kuthibitishwa mlipuko wa ugonjwa huo nchini Malawi.

Mpango wa dharura wa chanjo umeanza nchini Malawi ambapo matone ya chanjo yanawekwa kwenye midomo ya watoto nchini kote, ikiwa ni pamoja na katika mji mkuu, Lilongwe, na jiji kubwa zaidi la nchi hiyo, Blantyre.

Kampeni ya chanjo hiyo itapanuliwa siku ya Alhamisi na kujumuisha nchi jirani za Msumbiji, Tanzania na Zambia, kulingana na UNICEF ambayo inafanya kazi na serikali na washirika wengine.

Awamu tatu zaidi za chanjo zitafuata katika miezi ijayo kwa lengo la kuwafikia zaidi ya watoto milioni 20.

XS
SM
MD
LG