Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:21

Zambia: Lungu alaani kitendo cha utawala wa Hichilema kutwaa mali yake


Rais wa Zambia Hakainde Hichilema
Rais wa Zambia Hakainde Hichilema

Wakili wa rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu, amelaani hatua ya serikali ya nchi hiyo, kutwaa mali mbalimbali, zinazohusishwa na familia mwanasiasa huyo,na kusema kuwa kitendo hicho kimechochewa kisiasa.

Rais wa sasa wa Zambia amekuwa akikabiliana na ufisadi, lakini wakosoaji wanasema analenga wapinzani wake wa kisiasa.

Serikali ilitwaa rasmi mali hizo kutoka kwa familia ya Lungu wiki jana, ambazo ni pamoja majengo 15 za orofa mbili mbili, nyumba ya kulala wageni ya orofa tatu, shamba na nyumba ya kawaida. Mali hizo zilichukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Utaifishaji wa Mapato ya Uhalifu ya mwaka 2010, ambayo inaruhusu serikali kutwaa mali ambayo inaamini ilipatikana kwa njia zisizo halali.

Wakili wa Rais huyo wa zamani, Makebi Zulu, aliiambia VOA kwamba yeye wala wateja wake hawajapewa notisi ya mchakato wowote, ulio mbele ya mahakama yoyote kuhusu kukamatwa kwa mali hiyo.

Akizungumza na vyombo vya sheria tangu uchunguzi huo uanze mwaka jana, Zulu alisema wateja wake wametoa maelezo ya kutosha jinsi walivyopata mali hizo. Alisema serikali inazuia kwa makusudi taarifa hizo ili kuwaaibisha Lungu, mke wake Esther Lungu, na watoto wao.

Wakosoaji wa Rais Hakainde Hichilema (hah-kah-IHN-deh hee-chee-LAY-mah) wanasema tangu serikali yake ilipoanza kuwakamatwa viongozi wa utawala uliopita na kuwafanyia uchunguzi wa madai ya vitendo vya rushwa, hakuna yeyote kati yao aliyepatikana na hatia yoyote.

Hichilema anasisitiza kuwa vita dhidi ya ufisadi havina maana ya kuwadhulumu wapinzani wake wa kisiasa.

Forum

XS
SM
MD
LG