Afisa wa serikali amesema kwamba mafuriko yametokea na kuharibu barabara pamoja na makazi ya watu.
Jimbo la KwaZulu-Nathal linaendelea kushughulikia hasara kutokana na mafuriko ya mwezi uliopita, ambayo yalikuwa mabaya kuwahi kutokea kwenye jimbo hilo.
Mafuriko ya mwezi April yaliua watu 448, na wengine 6,800 kuachwa bila makazi, kando na kusababisha hasara ya miundo mbinu ya zaidi ya dola bilioni moja na nusu.
Mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa Afrika kusini, imeonya kutokea mvua kubwa katika miji kadhaa ikiwemo Durban, ambao ulikumbwa na mafuriko mabaya mwezi uliopita.
Wanasayanzi wanaamini kwamba pwani ya Afrika inaendelea kuwa katika hatari kwa dhoruba kali na mafuriko kutokana na ongezeko la uchafuzi gesi unalosababisha bahari hindi kuchemka.
Wanasayansi wameonya kwamba hali hiyo itaendelea kuwa mbaya zaidi katika miongo ijayo.