Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:54

Rais Ramaphosa ayaomba mashirika ya kimataifa kununua chanjo za Covid zinazotengenezwa Afrika


Rais Cyril Ramaphosa akitembelea kiwanda cha Aspen kinachotengeneza chanjo ya Covid 19, mjini Port Elisabeth, March 29, 2021. Picha ya AP
Rais Cyril Ramaphosa akitembelea kiwanda cha Aspen kinachotengeneza chanjo ya Covid 19, mjini Port Elisabeth, March 29, 2021. Picha ya AP

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Alhamisi ameyaomba mashirika ya kimataifa yanayosaidia katika mpango wa chanjo dhidi ya virusi vya corona kuanza kununua chanjo zinazotengenezwa Afrika, ili kampuni zinazotengeneza chanjo hizo zisisitishe uzalishaji kwa kukosa zabuni.

Nchi hiyo ya Afrika ambayo imeendelea kiviwanda iliongoza kampeni ya kutaka chanjo zitengenezwe katika bara la Afrika, na kuwa mtengenezaji wa kwanza na mkubwa wa chanjo ya Covid 19.

“Mashirika ya kimataifa ambayo yalipewa pesa nyingi za kununua chanjo kwa ajili ya nchi maskini hayanunui chanjo zilizotengenezwa Afrika, hata zile chanjo ambazo zinatumwa kwa nchi za Afrika,” Ramaphosa ameuambia mkutano wa kimataifa kuhusu Covid kwa njia ya mtandao.

“Hali hii lazima ibadilike,” Ramaphosa amesema katika hotuba yake kwa mkutano huo wa pili wa kimataifa kuhusu Covid ambao uliongozwa na Rais wa Marekani Joe Biden.

Kampuni kubwa ya Afrika Kusini ya kutengeneza dawa Aspen, wiki iliyopita ilitoa taarifa ya kusisimua kwamba haijapata zabuni yoyote ya chanjo ya Covid iliyotengenezwa Afrika kwa ajili ya Afrika, ambayo iliidhinishwa na kampuni ya Marekani Johnson and Johnson, na kutishia kufunga kiwanda chake cha uzalishaji isipokuwa tu ikipata zabuni.

XS
SM
MD
LG