Hili limekuja baada ya taarifa za kijasusi kuashiria kuwa Iran imehamisha makombora yake ya masafa ya mbali kwenda kwenye fukwe za nchi hiyo.
Hatua hiyo mara ya kwanza iliripotiwa na kituo cha televisheni cha CNN, ambapo ilikuwa ni ishara ya kwamba Iran inaweza kuwa inafikiria ama kujiandaa kushambulia vikosi vya Marekani, katika ukanda huo.
Afisa wa serikali aliyeongea na shirika la habari la Associated Press amesema hawakuwa na uhakika kwamba makombora hayo yaliyowekwa katika boti yalikuwa yakionyesha uwezo mpya wa kijeshi ama yalikuwa yakiihamishiwa kuelekea eneo jipya.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.