Akihudhuria mkutano wa awali wa kamati ya kuratibu ya Saudi Arabia na Irak huko Riyadhi, Tillerson alimwambia mfalme Salman wa Saudi Arabia pamoja na Waziri Mkuu wa Irak, Haider al-Abadi kwamba kuimarika kwa uhusiano wao kulionesha nia njema.
Alielezea kufunguliwa tena kwa mpaka mkubwa mwezi Agosti unaokatisha kati ya nchi hizo mbili na kuanza tena kwa ndege za moja kwa moja kati ya Bangladesh na Riyadh. Waziri Tillerson alisema wote mnawakilisha kuanza juu ya kile tunachotumaini kitakuwa mifululizo ya hatua mbadala za kuimarisha uhusiano na ushirikiano wenye nguvu juu ya masuala muhimu.
Ukuaji wenu wa uhusiano kati ya Saudi Arabia na Irak ni muhimu katika kuongeza nguvu zetu za pamoja za usalama na mafanikio na tunapata maslahi bora ndani yake. Mwanadiplomasia huyo wa cheo cha juu wa Marekani alisema Marekani inafuraha kuona mafanikio haya na inawasihi wote kupanua uhusiano huu muhimu kwa ajili ya uthabiti wa eneo.
Aliongeza pia Marekani ipo tayari kusimama kuuunga mkono kuendeleza uhusiano kati ya Saudi Arabia na Irak na tunawapongeza.