Katika ajali hiyo abiria wengine kadhaa walijeruhiwa. Ajali hiyo ilitokea karibu na mji wa Rahimyar Khan katika jimbo la mashariki la Punjab, maafisa wa Pakistan wamesema.
Picha za televijeni zimeonyesha moto mkubwa na watu walikuwa wanasikika wakilia.
Maafisa wa shirika la reli la Pakistan tayari wameanza kufanya uchunguzi juu ya tukio la ajali hiyo ya moto.
Taarifa za awali zimesema chanzo cha moto huo ni kulipuka kwa mitungi miwili ya gesi iliyokuwa ndani ya treni iliyokuwa inatumiwa na abiria kupikia.
Ajali za gari moshi hutokea mara nyingi nchini Pakistan, ambako shirila la reli limeshuhudia miongo kadhaa ya kuzorota kwa uboreshwaji wa usafiri wa reli kutokana na rushwa, utawala mbovu na ukosefu wa uwekezaji.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Patrick Nduwimana, Washington, DC.