Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:13

Abiria 42 wapoteza maisha Zimbabwe


Mji wa Gwanda ilipotokea ajali nchini Zimbabwe
Mji wa Gwanda ilipotokea ajali nchini Zimbabwe

Watu 42 wanahofiwa kufa katika ajali ya basi lililoshika moto kusini mwa Zimbabwe.

Watu 20 wamelazwa hospitali wakiwa na majeraha mabaya ya moto, kulingana na shirika la habari la Zimbabwe ZEC.

Picha zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii, zinaonyesha wafanyakazi wa shirika la msalama mwekundu wakiwaokoa waliojeruhiwa na kupelekea miili katika vyumba cya kuhifadia maiti.

Basi lililohusika katika ajali lilikuwa likisafiri kutoka mji wa Bulawayo kuelekea mji wa Beit-bridge liliposhika moto, katika kile kinatajwa kuwa hitilafu kwenye tenki la mafuta.

Wiki iliyopita, watu 50 waliaga dunia baada ya mabasi mawili kugongana ana kwa ana nchini Zimbabwe.

XS
SM
MD
LG