Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 07:54

Zaidi ya watu 130 wafa maji katika ajali ya feri Tanzania


Juhudi za uwokozi kwenye meli ya MV. Nyerere iliyozama kwenye ziwa Victoria
Juhudi za uwokozi kwenye meli ya MV. Nyerere iliyozama kwenye ziwa Victoria

Watu wasiopungua 130 waliripotiwa kufariki dunia kufikia Ijumaa huku wengine Zaidi ya 40 wakiokolewa baada ya kivuko cha MV Nyerere kuzama katika ziwa Victoria siku ya Alhamisi.

Ajali hiyo ya feri ilitokea katika wilaya ya Ukerewe nchini Tanzania. Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, George Nyamaha, alisema kivuko hicho kilikuwa na zaidi ya abiria 100 wakati wa ajali hiyo.

Shirika la habari la Reuters liliwanukuu maafisa wa serikali ya Tanzania wakisema kuwa wanahofia huenda watu zaid ya 200 wamepoteza maisha katika ajali hiyo.

Maafisa wa usafiri wanasema kuwa kirasmi, kivuko hicho cha MV Nyerere kinafaa kubeba abiria 100, tani 25 za mizigo na magari madogo matatu.

Picha ya maktaba ya meli ya MV Nyerere iliyozama Alhamisi
Picha ya maktaba ya meli ya MV Nyerere iliyozama Alhamisi

Hata hivyo, baadhi ya mashuhuda waliohojiwa na vyombo vya habari vya Tanzania walisema kwamba wakati wa ajali hiyo, feri hiyo ilikuwa imebeba watu wengi kupita kiasi.

Kufikia Alhamisi usiku, shughuli za uokoaji bado zilikuwa zikiendelea na huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka.

Baadaye, iliripotiwa kwamba shughuli za uokoaji zilisitishwa hadi kutakapopambazuka.

Feri hiyo imekuwa ikitoa huduma kwa watu wa Ukerewe tangu 2004.

Habari zaidi zitafuata...

XS
SM
MD
LG