Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 07:21

Serikali yaunda tume kuchunguza ajali ya MV Nyerere


Mwanamke akiwa na huzuni baada ya kumpoteza ndugu yake katika ajali ya MV Nyerere.
Mwanamke akiwa na huzuni baada ya kumpoteza ndugu yake katika ajali ya MV Nyerere.

Rais John Pombe Magufuli amemwondoa mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Mhandisi Dkt John Ndungura .

Taarifa ya Ikulu iliotolewa siku ya Jumatatu imeeleza kuwa Rais ameivunja bodi hiyo.

Magufuli alichukuwa uamuzi baada ya kuzama kwa Ferri - MV Nyerere Septemba 20, 2018, Ukerewe, Mkoani Mwanza, na kusababisha vifo vya watu 224, na matukio mbalimbali ya ajali za barabarani ambazo zimesababisha vifo, ulemavu na kuharibu mali.

Siku ya Jumapili, Rais Magufuli aliivunja bodi ya ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA) na kumfuta kazi Mwenyekiti wake John Ndunguguro kwa.

Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameteuwa tume ya watu saba ambayo itaanza uchunguzi juu ya ajali hiyo.

Tume hiyo inaongozwa na Mkuu wa Jeshi mstaafu George Waitara na Mbunge wa Upinzani kutoka eneo hilo Joseph Mkundi , aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Temesa, Mhandisi Celina Magessa na Wakili Julius Kalolo ambaye atasaidia mapitio ya sheria na mfumo mzima wa uendeshaji wa vivuko.

Tume hiyo imepewa mwezi mmoja kukusanya ripoti na kuiwasilisha kwa rais.

Pia Waziri Mkuu amesema serikali imeanza mipango ya kutengeza feri mpya ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba watu 200 na tani 50.

Kufikia sasa, serikali tayari imewakamata maafisa kadhaa waliokuwa wakifanya kazi katika Ferri hiyo.

XS
SM
MD
LG