Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 11:07

Ngome ya Buhari iko njia panda wakati uchaguzi umekaribia


Kampeni za uchaguzi katika jiji la Yola Nigeria, Februari 22, 2023. Picha na shirika la habari la REUTERS/Esa Alexander
Kampeni za uchaguzi katika jiji la Yola Nigeria, Februari 22, 2023. Picha na shirika la habari la REUTERS/Esa Alexander

Wakati mfanyabiashara wa viatu Haruna Abubakar alipompigia kura rais Muhammadu Buhari mwaka 2015 na kumpigia tena katika uchaguzi wa mwaka 2019, alikuwa miongoni mwa  wanigeria zaidi ya milioni moja wanaomuunga mkono aliyekuwa mkuu wa jeshi kwenye ngome yake ya Kaskazini katikaa Jimbo la Kano.

Ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Nigeria na kitovu cha uchumi kwa Waislamu wa upande wa kaskazini mwa nchi hiyo, Kano lilikuwa jimbo muhimu lililompatia ushindi na miaka minne baadaye kuchaguliwa tena kutokana na ahadi zake pacha za kupambana na wanajihadi na rushwa.

Baada ya kumpa rais Buhari nafasi mara mbili ya kumchagua, Abubakar alisema amekata tamaa kuhusu uwezo wa chama chake tawala cha All Progressives Congress APC, kwa hiyo atampigia kuwa mgombea wa chama kingine katika uchaguzi wa urais utakaofanyika Jumamosi.

Kwa muda mrefu Kano imekuwa ngome ya Buhari, wa kabila la Fulani kutoka katika jimbo jirani la Katsina. Sasa anaondoka madarakani, kundi kubwa la wapiga kura waliomsaidia kushinda mara mbili hawana uhakika nani wa kumpigia kura.

“Tumempa nafasi mara mbili tukidhani mambo yatabadilika na kuwa mazuri zaidi” alisema Abubakar kuhusiana na kura zake alizompigia Buhari “Lakini mambo yamekuwa kinyume – kuna ukosefu zaidi wa usalama na watu wako katika hali ngumu”.

Zaidi ya Wanigeria milioni 93 wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Februari 25, wakati nchi yao inakabiliwa na ukosefu mkubwa wa usalama kutoka kwa wanajihadi, magenge ya wahalifu na makundi ya wanaotaka kujitenga, mfumuko wa bei ambao uko katika tarakimu mbili, ukosefu wa ajira na kuongezeka kwa umaskini.

Chanzo cha habari hii ni Agence France-Presse AFP

XS
SM
MD
LG