Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:12

Maafisa saba wa polisi wauawa Nigeria


Polisi wa Nigeria. Picha ya AP ya Februari 16, 2023
Polisi wa Nigeria. Picha ya AP ya Februari 16, 2023

Watu wenye silaha  mwishoni mwa wiki wamewaua maafisa saba wa polisi nchini  Nigeria katika eneo la kusini mashariki, msemaji wa polisi amesema Jumanne, katika  ghasia  za karibuni zilizoukumba mkoa  tete kabla ya uchaguzi wa Jumamosi.

Kusambaa kwa ukosefu wa usalama ni miongoni mwa wasi wasi mkubwa kwa wanigeria katika kipindi hiki wanachoelekea kwenye uchaguzi wa wabunge wapya na mrithi wa rais Muhammadu Buhari.
Katika eneo la kusini mashariki, ghasia zinazofanywa na magenge yenye silaha na makundi ya washukiwa wanaotaka kujitenga, zimeuwa dazeni ya watu mwaka huu na kuzishambulia ofisi za tume ya uchaguzi , vituo vya polisi na majengo ya serikali.

Msemaji wa polisi wa jimbo la Anambra, Ikenga Tochukwu, alisema maafisa watatu wa polisi waliuwawa baada ya watu wenye silaha kutumia vilipuzi walivyotengeneza na kufyatua risasi katika kituo cha polisi katika eneo la serikali za mitaa la Idemili.

Siku ya Jumamosi na Jumapili, watu wenye silaha walitumia mabomu ya petroli na bunduki kuvishambulia vituo wiwili vya polisi na kuua maafisa wanne katika maeneo ya serikali za mitaa ya Idemili na Oyi, Tochukwu aliongeza.

Amesema washukiwa wanachama wa kundi linalotaka kujitenga Biafra (IPOB) walihusika na mashambulizi hayo. IPOB, ambalo serikali ya Buhari imelitaja kuwa ni kundi la kigaidi limekanusha kuhusika na shambulizi.


Chanzo cha habari hii kinatoka Shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG