Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:17

Mgombea urais Peter Obi anaongoza takriban kura tano za maoni Nigeria


Mgombea urais wa chama cha Labour, Peter Obi akiwahutubia wafuasi wake wakati wa mkutano wake wa kampeni, kuelekea uchaguzi wa urais wa Nigeria huko Lagos Nigeria, Februari 11, 2023. REUTERS
Mgombea urais wa chama cha Labour, Peter Obi akiwahutubia wafuasi wake wakati wa mkutano wake wa kampeni, kuelekea uchaguzi wa urais wa Nigeria huko Lagos Nigeria, Februari 11, 2023. REUTERS

Raia wa Nigeria watapiga kura siku ya Jumamosi katika mchuano unaoweza kuwa wa kuaminika na wa karibu zaidi wa uchaguzi tangu utawala wa kijeshi uliomalizika karibu robo karne iliyopita  na wa kwanza ambapo mgombeaji wa urais ambaye hatoki katika mojawapo ya vyama viwili vikuu anapata nafasi.

Aliyekuwa gavana wa Lagos, Bola Tinubu wa chama tawala cha All Progressives Congress (APC) anachuana na Atiku Abubakar wa chama kikuu cha upinzani cha Peoples Democratic Party (PDP) na Peter Obi, mgombea ambaye ameibukia kuwa maarufu ambaye alikihama chama cha PDP na kujiunga na chama kidogo cha Labour na sasa anaongoza takriban kura tano za maoni.

Obi, mwenye 61, ametumia kampeni ya mitandao ya kijamii kuhamasisha kura za vijana wanaozidi kutoridhika, waliochoshwa na siasa za zilizozoeleka na wazee ambao wana mwelekeo wa kuwatawala na Tinubu na Abubakar wote wako katika miaka ya 70.

Lakini wachambuzi wanahoji kama kura za maoni zinazomweka mbele ni za kutegemewa na wanatambua kwamba hana rasilimali au msingi mkubwa wa kisiasa uliojengwa kwa miongo kadhaa ambayo wengine wawili wanayo.

Yeyote Wanigeria watakayemchagua kumrithi Rais Muhammadu Buhari ambaye ni wa pili tu katika historia ya Nigeria kuacha kugombea kwa hiari baada ya kutumikia mihula miwili ya kidemokrasia atalazimika kutatua msururu wa migogoro ambayo imekuwa mibaya zaidi chini ya utawala wa jenerali huyo mstaafu wa jeshi.

XS
SM
MD
LG