“Msafara wa kikosi cha MINUSMA ulikanyaga bomu la kujitengenezea,” MINUSMA imesema kwenye Twitter na kutoa idadi ya awali ya wanajeshi watatu waliofariki na wengine watano kujeruhiwa vikali.
Mali inakabiliwa na uasi wa miaka 11 wa wanamgambo wa kiislamu ambao umeua maelfu ya watu na kulazimisha maelfu ya wengine kuhama makazi yao.
Afisa wa Umoja wa mataifa ambaye hakutaka jina lake litajwe amethibitisha kwamba walinda usalama hao walikuwa wa kikosi cha Senegal kinachoshiriki kwenye tume ya MINUSMA.