Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:16

Mgombea Urais aahidi kuleta matumaini Nigeria


Mgombea urais wa chama tawala cha All Progresive Congress APC, Bola Ahmed Tinubu (kushoto) akiwa na Kashim Shettima Julai 20, 2022. (Picha na Kola Sulaimon / AFP)
Mgombea urais wa chama tawala cha All Progresive Congress APC, Bola Ahmed Tinubu (kushoto) akiwa na Kashim Shettima Julai 20, 2022. (Picha na Kola Sulaimon / AFP)

Mgombea urais wa chama tawala nchini  Nigeria Bola Tinubu ameahidi kurejesha matumaini kwa wale wanaopoteza imani nchini humo endapo atachaguliwa.

Taifa hilo lenye demokrasia kubwa sana barani Afrika ambalo pia linakabiliwa na ukosefu wa usalama na mzozo mkubwa kiuchumi litafanya uchaguzi wake mkuu jumamosi.

Tinubu, anayetazamiwa na wengi kushinda uchaguzi wenye mchuano mkali, alizungumza katika mkutano wake wa mwisho wa chama chake cha All Progressives Congress, APC katika uwanja wa michezo ambao ulikiwa mtupu kwa theluthi mbili, huko mjini Lagos, kitovu cha biashara ambako aliwahi kuhudumu kama gavana.

Wakicheza ngoma za kitamaduni na wakiwa wamevaa nguo zenye picha yake , wafuasi wengi wa Tinubu walisifu mafanikio yake ya kuubadilisha mji huo wakati alipokuwa kiongozi na baadaye aliteuliwa kuwa mrithi aliwania wadhifa huo na kuliongoza jiji hilo kati ya mwaka 1999 na 2015.

Lakini Tinubu pia ameshutumiwa kuwa na "mahusiano" na wanasiasa wengine, akitumia nafasi yake kwa siri na kuhatarisha demokrasi.

Akiwa pamoja na Rais Muhammadu Buhari, ambaye sehemu kubwa ya urais wake ukigubikwa na mzozo wa usalama ulioenea takriban nchi nzima, ambao umesababishwa na kuzuka kwa makundi yenye silaha yanayo sababisha kuenea kwa machafuko nchini kote.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG