Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:48

Raia 10 wauwawa na Al Shabab, Somalia


Wapiganaji  wa kundi la Al-Shabaab walishambulia nyumba moja katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, Jumanne, na kuua raia kumi kwa mujibu wa serekali. 

Uvamizi huo ulifanyika majira ya saa nane mchana kwa saa za huko katika wilaya ya kaskazini ya Abdiaziz, serikali ilisema na kuongeza kuwa raia watatu wamejeruhiwa.

Imeongeza kusema kwamba vikosi vya usalama viliwaokoa na kuwatoa raia wengine kwenye nyumba hiyo na majengo mengine ya karibu wakati wa shambulizi.

Kundi la Al Shabab ambalo lina uhusiano na Al Qaeda, lilitangaza kuhusika na shambulio hilo.

Mwanajeshi aliyetajwa kwa jina la Mohamed Ali, ambaye alikuwepo eneo la tukio, alisema washambuliaji walilivamia jengo baada ya kulipua lango kuu kwa vilipuzi.

Amesema wanajipanga kushambulia nyumba wanazo ishi raia baada ya kushindwa katika uwanja wa mapambano.

Katika miezi ya hivi karibuni jeshi la Somalia na wanamgambo wa koo wamekomboa sehemu kadhaa za maeneo kutoka kwa wanamgambo hao katika operesheni inayo saidiwa na mashambulizi ya anga ya Marekani na kikosi cha Umoja wa Afrika kinachojulikana ATMIS.

Lakini Al-Shabaab, ambayo imekuwa ikipigana na serikali tangu 2007, bado inadhibiti sehemu mbalimbali za nchi ambako wamefanya mashambulizi mengi ya kulipiza kisasi nchini humo na katika nchi jirani.

Katika shambulio baya zaidi la Al-Shabaab tangu mashambulizi dhidi yao kuanzishwa mwaka jana, watu 121 waliuawa katika milipuko miwili ya mabomu yaliyotegwa kwenye gari katika wizara ya elimu mjini Mogadishu mwezi Oktoba.

XS
SM
MD
LG