Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:04

Sababu za Jill Biden kuzuru Namibia na Kenya


 Jill Biden asalimiana na rais wa Namibia Hage Geingob alipowasili nchini humo Jumatano Februari 22, 2023 kuanza ziara ya siku tano barani Afrika.
Jill Biden asalimiana na rais wa Namibia Hage Geingob alipowasili nchini humo Jumatano Februari 22, 2023 kuanza ziara ya siku tano barani Afrika.

Jill Biden, mke wa Rais wa Marekani Jumatano aliwasili Namibia kuanza ziara yake ya siku tano katika bara hilo ambayo itampeleka hadi nchini Kenya.

Akiwa huko, Bi Biden atalenga kuhusu uwezeshaji wanawake, masuala ya watoto na ukosefu wa usalama a chakula ambao umelikumba eneo kubwa la bara hilo.

Jill Biden alilitembea bara hilo mara tano wakati mume wake alipokuwa makamu wa rais, aliangazia ya wale wasiokuwa na nguvu. Alizungumzia kuhusu kambi kubwa sana ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya mwaka 2011.

“Kina mama wanawapeleka watoto wao kutoka Somalia, wanatembea mara nyingine siku 15, 20, 25 na wanawapoteza wakiwa njiani, watoto wao hufariki. Kwahiyo ninachosema ni kwa wamarekani je huenda tunaweza kuwafikia na kuwasaidia kwasababu hali ya huko ni mbaya sana,” alisema.

Hivi sasa mke wa rais, anarejea nchini Kenya wiki hii. Hivi leo atakuwa nchini Namibia, ikiwa ni mara ya kwana kwa mke wa rais kufanya hivyo tangu taifa hilo lijipatie uhuru miongo mitatu iliyopita.

Kwa kuongezea, atalenga zaidi masuala ya wanawakena watoto, mke wa rais pia ataangazia suala ya ukosefu mkubwa wa usalama wa chakula, hali ambayo inawagubika tena eneo la Afrika Mashariki.

Mwezi Desemba, Rais Biden alitangaza msaada wa kibinadamu wa takriban dola bilioni 2 ili kupambana na tatizo hilo katika eneo kanda hiyo.

“Msaada huu utasaidia kuhakikisha kwamba watoto na familia hawalali na njaa,” Joe Biden alisema.

Ziara za mke wa rais mara nyingi zinatoa mbinu kwa mkakati na mwelekeo wa urais – kwa kiasi kwasababu, wakati Jill Biden mwenyewe anaelezea wazi kuwa hana mamlaka ya kiutendaji na hana mamlaka kutoka kwa wapiga kura wa Marekani.

“Sijachaguliwa – lakini nilikuwa najukumu fulani. Kama wake wa wakubwa, tunawahudumia watu katika nchi zetu. Si ndiyo? Tunaona mioyo yao na matumaini. Tunashuhudia miujiza midogo ya huruma na ukarimu kati ya majirani. Tunafahamu kitu gani kinaweza kutokea wakati jamii zinapokuja pamoja – mangapi yanaweza kubadilika wakati tunafanya kazi kushughulikia sababu ambazo ni kubwa kuliko sisi wenyewe,” alisema.

Wake wa marais wa Marekani kwa kawaida wanapokelewa vizuri sana barani Afrika, amesema Katherin Jellison, profesa wa Marekani wa masuala ya historia ya wanawake na jinsia katika chuo kikuu cha Ohio – pengine kwasababu wana fursa nzuri kwa rais.

Kwa kweli kutakuwa na ukaribisho mzuri kwa mtu ambaye si mwanasiasa ambaye anafanya kuliko mwanasiasa, kwasababu huenda kungekuwa na masharti fulani,” alisema Katherine Jellison wa Chuo Kikuu cha Ohio.

Wakati huo huo, utawala wa Biden umekuwa ukiieleza Afrika kuhusu kuiunga mkono Ukraine dhidi ya Russia na hivi karibuni waziri wa fedha Janet Yellen alikwenda Senegal, Zambia na Afrika Kusini.

Na waziri wa mambo ya nje wa Russia mwaka huu alifanya ziara kadhaa katika mataifa ya Afrika ambayo yana historia au yenye uhisiano wa kiitkadi na Russia au iliyokuwa Umoja wa Sovieti, kama Mali, Sudan na Angola.

China imempeeka waziri wake mpya wa mambo ya nje barani Afrika katika ziara yake ya kwanza huko – ikiwa ni dalili ya maslahi ya kina ya taifa hilo barani humo.

Mke wa rais atakuwepo barani humo kwa siku tano.

XS
SM
MD
LG