Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 09:41

Biden atangaza msaada wa ziada kwa waathirika wa Kimbunga Ian Florida


Rais wa Marekani Joe Biden (kushoto) akiwa na Gavana wa Florida Ron DeSantis
Rais wa Marekani Joe Biden (kushoto) akiwa na Gavana wa Florida Ron DeSantis

Rais Joe Biden jana Jumatano alielekea kwenye jimbo lililokumbwa na kimbunga la Florida,  akikutana na mmoja wa wakosoaji wake,  Gavana Ron DeSantis.

Biden aliahidi kuongeza msaada kwa jimbo hilo maarufu kama Sunshine State, wakati gavana akipongeza ushirikiano wa serikali ya jimbo na serikali kuu. Mwandishi wa VOA Anita Powell anaripoti kutoka Washington.

Upepo mkali, kuendesha gari huku mvua inanyesha na kusambaa kwa uharibifu.

Kikilaumiwa kimbunga Ian, cha hatua ya 4 ambacho kiliipiga Florida wiki iliyopita, na kuua zaidi ya watu 100 na majengo ya mabilioni ya dola katika jimbo hilo kuharibiwa vibaya na mafuriko.

Uharibifu wa makazi ya watu uliyotokana na Kimbunga Ian.
Uharibifu wa makazi ya watu uliyotokana na Kimbunga Ian.

Jumatano, Rais Joe Biden alitembelea mabaki ya uharibifu kwenye eneo la Fort Myers, eneo la ufukweni lenye kiasi cha wakazi 87,000. Mji huo ambao kwa kiasi kikubwa una warepublican wengi ni moja ya vituo ambavyo vinakua sana kwa ongezeko la idadi ya watu.

Biden alisema kuwa serikali kuu ina nia ya dhati kumsaidia kila mmoja aliyeathiriwa, na kutangaza msaada wa ziada wa serikali kuu kwa kipindi cha siku 60.

Msaada huo unahusisha gharama za utafutaji na kuokoa, makazi, chakula na hatua nyingine za dharura za kuokoa maisha.

Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza na wakazi wa Florida kuhusu juhudi za msaada wa serikali kuu kwa wakazi wa Florida wakati akitembelea maeneo yaliyoharibiwa na kimbunga Ian katika ziara yake Florida, Octoba 5, 2022. Wakwanza kulia ni Gavana wa Florida Ron DeSantis aliyekuwa akizunguka naye na pia mkewe Jill alifuatana naye katika ziara hiyo.
Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza na wakazi wa Florida kuhusu juhudi za msaada wa serikali kuu kwa wakazi wa Florida wakati akitembelea maeneo yaliyoharibiwa na kimbunga Ian katika ziara yake Florida, Octoba 5, 2022. Wakwanza kulia ni Gavana wa Florida Ron DeSantis aliyekuwa akizunguka naye na pia mkewe Jill alifuatana naye katika ziara hiyo.

Rais wa Marekani, Joe Biden alieleza: “Hivi leo tuna kazi moja, kazi moja pekee. Nayo ni kuhakikisha kwamba kila mtu hapa Floria anapata kila kitu ambacho anakihitaji kwa ukamilifu wakati wote huu wa dharura hii. Sisi ni moja ya mataifa machache duniani ambayo katika msingi wa mzozo tunaokabiliwa nao, sisi ni taifa pekee ambalo limetoka katika hili likiwa vizuri kuliko ilivyokuwa.”

Gavana wa Florida Ron DeSantis, mrepublican na mmoja wa wakosoaji wakali na mwenye nguvu wa Biden, amewapongeza wahusika kwa ushirikiano wao.

Katika matamshi yake mafupi, hakumtaja Biden kwa jina.

Ron DeSantis, Gavana wa Florida alisema: “Nadhani moja ya mambo ambayo mnayaona katika majibu haya, tunapunguza urasimu. Tunapungua kupitia urasimu kuptia ule wa serikali za majimbi, serikali za kuu, hadi kwa rais. Kwahiyo tunashukuru kwa juhudi hizi za pamoja.”

Katika jamii za kidemokrasia, viongozi waliochaguliwa kushughulia dharura za majanga wanaonyesha jinsi serikal inavyowahudumia watu.

Andrew Reeves wa chuo kikuu cha Washington anasema “Wapiga kura kwa kweli wanajaibu jinsi rais anavyochukua hatua, au gavana anavyochukua htua, kwa njia ambayo ni kubwa ya majibu, kama vile ni kitendo kisicho cha kwaida kutoka kwa mwenyenzi mungu kilichosababisha uharibifu mkubwa hapo awali.”

Uharibifu uliyosababishwa na Kimbunga Ian katika eneo la Fort Myers, Florida.
Uharibifu uliyosababishwa na Kimbunga Ian katika eneo la Fort Myers, Florida.

DeSantis ambaye anawania katika uchaguzi wa katikati ya awamu, katika jimbo hilo lenye utajiri, huenda ukawa ni mmoja mtihani wake alisema.

Andrew Reeves wa chuo kikuu cha Washington anasema “wapiga kura hawatayaangalia mambo haya kwa miezi sita ijayo, mwaka mmoja, miaka miwili baada ya uchaguzi. Lakini DeSantis anawania kuchaguliwa tena.na hili linatokea, unafahamu wakati huu. Kwa hiyo, kama mnavyofahamu yeye ni kiongozi maarufu wa kisiasa, nadhani, katika muktadha huu tutaona atakavyoibuka baada ya yote kusema na kutekelezwa.”

Lakini uchaguzi wa katikati ya awamu pengine siyo kipaumbele kikubwa sana kwa watu wa Florida.

“Lakini tunafahamu hisia zenu” hizo kuhusu wapi nitakiweka kichwa changu kwenye mto usiku ukiingia? Nitakwendaje kazini? Je mtoto wangu atakuwa salama?, alisema Rais Biden.

Jumatano, watu hawa wawiali wamegawanyika kisiasa, walisema kwa sauti moja kuwa mambo yatakuwa sawa.

XS
SM
MD
LG