Zaidi ya watu 200 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko na maporomoko ya matope huko Afrika Mashariki tangu kuanza kwa msimu wa mvua, ambao bado haujakwisha.
Watalaamu wanasema mvua zimekuwa kubwa mno mwaka 2019 kutokana na kile kinachoitwa Indian Ocean Dipole hali ambayo inasababisha viwango vya juu wa joto katika maji kwenye bahari ya Hindi na kupanda kwa digrii mbili celcius.
Watu wengi wamepoteza maisha, na nusu kati ya hao ni huko nchini Kenya. Mvuvi mmoja, Vincent Musila ambaye aliokolewa baada ya kukwama kwenye kisiwa kidogo kwa takriban siku tatu anaelezea hali iliyomkuta.
"Nilikwenda huko siku ya Ijumaa kwa ajili ya kuvua. Nilipokuwa naelekea huko kulikuwa hakuna maji. Ghafla maji yalijaa na katika muda wa dakika mbili, nilizungukwa na maji na sikuweza kwenda popote," amesema Musila.
Pia amesema : "Nyumba na mazao yameharibiwa. Barababara na madaraja yameharibiwa, imekuwa vigumu kufika katika vijiji vya ndani kabisa na kugawa misaada. Wakazi wanaondoka katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko kwenda katika maeneo makavu."
Joseph Otieno Abogo mkazi wa Kakola Ombaka, nchini Ethiopia, ambaye hivi karibuni alimzika mke wake anakhofia kuwa maji ya mafuriko huenda yakafukua jeneza la kutoka katika kaburi.
Mkazi mwingine David Aguko raia wa Ethiopua ambaye amepoteza nyumba yake katika mafuriko hayo anaelezea yaliyomsibu.
Wakati huohuo mvua kubwa zimesababisha mafuriko mabaya katika sehemu za Sudan Kusini na kuzilazimisha jamii ambazo ziliwahi kukoseshwa makazi kutokana na ghasia kuhama tena. Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini katika eneo la Akobo inajitahidi kutoa huduma za msingi kwa maelfu ya watu walioathiriwa na mafuriko.
Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, David Shearer anasema: Eneo hili hapa liko nyanda za chini. Maji yanakuja kutoka Ethiopia pia. Kwa kweli ni janga. Tutarejea, tutazungumza na wale ambao wanatoa misaada ya kibinadamu.
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, tayari limepeleka chakula kupitisha shirika la hisani la Uingereza Oxfam. Lakini mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kwa Sudan Kusini anasema kiwango kinachohitajika ni kikubwa mno kuliko ambavyo tulifikiria.
Shearer anaongeza kuwa: "Ndiyo tunaweza kutoa msaada wa dharura hivi sasa, lakini watu hawa wanategemea au wamekuwa wakitegemea mavuno kwa mika mingi. Mavuno hayo huenda yakaathiriwa vibaya kwahiyo kuna chakula kidogo kuliko kile ambacho wamekipanda wenyewe, kwahiyo huenda wakawa wategemezi zaidi wa chakula kutoka nje."
Mvua ni jambo la kawaida Afrika Mashariki kati ya October na December, lakini si nyingi kiasi hiki. Wanasayansi wanalaumu mvua kubwa zisizo za kawaida ni kwa sababu ya viwango vya juu vya joto kwenye bahari ya Hindi. Na hivyo kupelekea maji kutoa mvuke na hatimaye kusababisha mvua nyingi kuliko kawaida.