Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:17

Maporomoko ya ardhi yasababisha vifo vya watu 36 magharibi mwa Kenya


Maporomoko ya ardhi Pokoto Magharibi Kenya Nov 23, 2019
Maporomoko ya ardhi Pokoto Magharibi Kenya Nov 23, 2019

Juhudi za uwokozi zimekwama kutokana na barabara kugeuka mito ya maji na daraja kuharibiwa. Waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i amesema helikopta za polisi zimepelekwa kusaidia.

Mafisa wa usalama wa Kenya wamethibitisha kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na tukio la maporomoko ya udongo katika kaunti ya Pokot Magharibi kwenye mpaka na Uganda, imefikia 36.

Hii ni baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko iliyotokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika eneo hilo. Kamishna wa kaunti Apollo Okello ameliambia gazeti la Daily Nation kwamba wameweza kupata miili ya watu 12 wakiwemo watoto 7. Okelleo anasema watoto wawili wameokolewa wakiwa hai.

Juhudi za uwokozi zimekwama kutokana na barabara kugeuka mito ya maji na daraja kuharibiwa na mafuriko.

Maporomoko hayo yameathiri zaidi vijiji vya Nyarkulian na Parua, ambavyo vinasemekana kutenganishwa baada ya daraja kusombwa na mafuriko.

Waziri wa mambo ya ndeni ya Kenya Fred Matiang’i akizungumza na shirika la habari la AFP, ametowarambi ramfi kwa familia walopoteza jamaa zao na kueleza kwamba helikopta za polisi zimepelekwa katika katika Kaunti hiyo kusaidia juhudi za uwokozi.

XS
SM
MD
LG