Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 20:25

Marekani: Mshauri wa usalama wa taifa akanusha taarifa kuwa Saudia na Israeli wanakaribia kufikia makubaliano


Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu (kushoto) na Mwana mfalme Mohammad Bin Salman.
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu (kushoto) na Mwana mfalme Mohammad Bin Salman.

Mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani Jake Sullivan aliweka matumaini madogo  kwa mkataba wa Saudia Arabia na Israel wa kurejesha uhusiano wa kawaida  ambao Washington unaufanyia kazi, akitupilia mbali habari zinazopendekeza kuwa  makubaliano yanakaribia kukamilika.

“Bado kuna njia kadhaa kuhusiana na vipengele vyote vya majadiliano hayo,” Sullivan alisema wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Jumanne.

Katika miezi iliyopita, Sullivan na manaibu wake wameanza mashauriano ya pembeni na Wasaudi na Waisraeli kwa ajili ya kuweka msingi kwa makubaliano hayo.

Amani kati ya nchi hizo mbili itakuwa ni “suala muhimu” na manufaa kwa Marekani “kwa namna ya kimsingi,” Sullivan alisema, akieleza kuwa lengo hilo la “muungano zaidi, na Mashariki ya Kati iliyo thabiti zaidi” ambapo nchi zitaweza kushirikiana “kwa kila kitu kuanzia uchumi hadi teknolojia na usalama wa kikanda.”

Hakutaka kutoa maoni yake kuhusu uwezekano wa mkutano baina ya Rais Joe Biden na Mwana mfalme Mohammad Bin Salman pembeni ya mkutano wa viongozi wa G20 huko New Delhi mwezi ujao.

Mazungumzo juu ya kurejesha uhusiano yalianza chini ya uongozi wa Rais Donald Trump, ambaye aliishinikiza Saudi Arabia kujiunga na nchi nyingine za Kiarabu – Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Morocco – kusaini mikataba iliyosimamiwa na Marekani ya Abraham Accords inayoitambua Israeli.

Rais wa Marekani Joe Biden alipokutana na Mwana mfalme Mohammed bin Salman Saudi Arabia Julai 15, 2022. (Bandar Aljaloud/Saudi Royal Palace via AP, File)
Rais wa Marekani Joe Biden alipokutana na Mwana mfalme Mohammed bin Salman Saudi Arabia Julai 15, 2022. (Bandar Aljaloud/Saudi Royal Palace via AP, File)

Tangu kupatikana Mikataba hiyo, mahusiano ya Riyadh na Israeli yameboreka, na kumuwezesha Biden Julai 2022 kuwa rais wa kwanza wa Marekani kusafiri moja kwa moja kwenda Jeddah akitokea Tel Aviv baada ya Ufalme wa Saudi Arabia kufungua anga zake kwa ndege zinazotoka na kwenda Israeli.

Forum

XS
SM
MD
LG