Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 08:50

Ethiopia kuchunguza mauaji ya raia wake kwenye mpaka wa Saudi Arabia


Mtoto aliyerejeshwa Ethiopia kutoka Saudi Arabia, baada ya kushuka kwenye ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole mjini Addis Ababa Aprili 1, 2022. Picha na REUTERS/Tiksa Negeri
Mtoto aliyerejeshwa Ethiopia kutoka Saudi Arabia, baada ya kushuka kwenye ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole mjini Addis Ababa Aprili 1, 2022. Picha na REUTERS/Tiksa Negeri

Ethiopia itaanzisha uchunguzi wa pamoja na Saudi Arabia kuhusu ripoti ya Human Rights Watch inayowashutumu walinzi wa mpaka wa taifa hilo la kifalme kuua mamia ya wahamiaji kutoka Ethiopia, wizara ya mambo ya nje imesema Jumanne.

"Serikali ya Ethiopia itafanya uchunguzi haraka kuhusiana na tukio hilo sambamba na maafisa wa Saudi Arabia," wizara hiyo ilisema kupitia mtandao wa X, uliyokuwa Twitter, siku moja baada ya kuchapishwa kwa ripoti ya HRW ambayo imezusha hasira katika pembe zote za dunia.

"Katika wakati huu tete, inashauriwa sana kujizuia kueneza uvumi hadi hapo uchunguzi utakapokamilika," wizara ilisema, ikibainisha "uhusiano mazuri ya muda mrefu" kati ya Addis Ababa na Riyadh.

Madai hayo ambayo yameelezwa kuwa " hayana msingi" na afisa wa serikali ya Saudi Arabia yanamulika kuongezeka kwa unyanyasaji katika njia hiyo hatari inayotokea Pembe ya Afrika kwenda Saudi Arabia, ambako maelfu ya Waethiopia wanaishi na kufanya kazi.

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 20 kutoka jimbo la Oromia nchini Ethiopia, aliyehojiwa na HRW, akisema kwamba walinzi wa mpakani wa Saudi Arabia waliwafyatulia risasi kundi la wahamiaji ambao waliachiliwa kutoka kizuizini muda mfupi kabla.

"Walitufyetulia risasi kama mvua. Nikikumbuka, nalia," alisema.

Washington ambaye ni mshirika wa muda mrefu wa Riyadh, imehimiza "uchunguzi wa kina na wa uwazi" ufanyike kuhusiana na tuhuma hizo, ambazo hazikupewa uzito na afisa wa serikali ya Saudi Arabia wakati alipozungumza na shirika la habari la AFP.

Shirika hilo la HRW lenye makao yake mjini New York limekuwa likiorodhesha unyanyasaji dhidi ya wahamiaji wa Ethiopia nchini Saudi Arabia na Yemen kwa kipindi cha takriban muongo mmoja sasa.

Chanzo cha nabari hii ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG