Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 11:30

Hali ya tahadhari yatangazwa kwenye mkoa wa Ethiopia wa Amhara


Picha ya mji wa Lalibela, uliopo mkoa wa kaskazini wa Amhara
Picha ya mji wa Lalibela, uliopo mkoa wa kaskazini wa Amhara

Baraza la mawaziri la Ethiopia limetangaza hali ya dharura katika  mkoa wa Amhara, baada ya mamlaka kuomba msaada kufuatia kuongezeka kwa mapambano kati ya vikosi vya kieneo na jeshi la serikali.

Ofisi ya waziri mkuu imetangaza hali hiyo mapema leo baada ya viongozi wa kieneo kusema kwamba mafisa wa usalama wameshindwa kudhibiti hali, ingawa bunge linahitaji kuidhinisha hatua hiyo.

Tangazo hilo limesema kwamba “Tishio lililopo linahujumu usalama wa kitaifa na kuvuruga amani ya umma kila uchao.” Uchumi pia unasemekana kuathirika wakati makundi yenye misimamo mikali yakilaumiwa.

Mkoa wa Amhara ambao ni wa pili kwa wingi wa watu nchini Ethiopia umekumbwa na misukasuko tangu Aprili, pale vikosi vya serikali vilipoanza kupokonya silaha kutoka kwa vikosi vya kieneo, kufuatia kumalizika kwa vita vya mkoa jirani wa Tigray.

Serikali kuu pia ilijarubu mwaka jana kuvunja kikosi kisicho rasmi cha Amhara kwa jina Fano.

Forum

XS
SM
MD
LG