Waziri wa mambo ya nje wa Japan kufuatia mkutano wake wa ana kwa ana na naibu waziri mkuu wa Ethiopia alielezea matumaini kuwa mataifa yao mawili yatafanya kazi pamoja katika kurejesha mpango wa Nafaka wa Black Sea.
Waziri wa mambo ya nje wa Japan Yoshimasa Hayashi katika ziara yake ya kwanza nchini Ethiopia siku ya alhamisi alieleza matumaini yake kuwa nchi hizo mbili zinaweza kufanya kazi pamoja ili kurejesha tena mpango wa nafaka wa Black Sea.
Waziri huyo wa mambo ya nje ameelezea wasi wasi wake kuhusu uchokozi wa Russia dhidi ya Ukraine katika suala la usalama wa chakula Afrika katika mkutano na naibu waziri mkuu wa Ethiopia.
Tangu kuanza kwa mkataba wa nafaka wa Black Sea ambao ulianza kutumika Julai 2022. Umoja wa Mataifa umesimamia usafirishaji wa zaidi ya tani 262 za ngano kwenda Ethiopia.
Majanga ya hali ya hewa ambayo yalileta ukame na mizozo nchini Ethiopia yamesababisha zaidi ya watu milioni 20 kuhitaji msaada wa chakula.
Hayashi pia alizungumzia kuhusu uungaji mkono wa serikali ya Japan katika makubaliano ya amani ambayo yalileta mwisho wa vita katika eneo la Tigray nchini Ethiopia.
Demeke ambaye pia anahudumu kama waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia alisema wawili hao walikuwa na majadiliano yenye tija kuhusu masuala yenye maslahi kwa pande zote mbili.
Ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Japan Kusini Magharibi mwa Asia na Afrika ilihitimishwa Alhamisi nchini Ethiopia baada ya hapo awali kupitia katika nchi za Afrika Kusini na Uganda.
Forum