Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 17:54

Ethiopia kuanza kutumia huduma ya M- pesa


Wakazi wa kijiji cha Nyang'oma Kogelo huko Kenya, alikotoka baba wa aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama. Picha na REUTERS/Thomas Mukoya.
Wakazi wa kijiji cha Nyang'oma Kogelo huko Kenya, alikotoka baba wa aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama. Picha na REUTERS/Thomas Mukoya.

Huduma ya kupokea na kutuma pesa kwa njia ya simu ya M-Pesa imeanza kutumika nchini Ethiopia siku ya Jumatano, ikiwa ni msukumo kwa kampuni ya mawasiliano ya Kenya inayojaribu kuanzisha ukuaji wa huduma hiyo katika mojawapo ya nchi zenye uchumi mkubwa sana barani Afrika.

Sehemu ya kampuni ya Safaricom inayomilikiwa na kampuni ya Vodacom ya Afrika Kusini na Vodafone ya Uingereza, imezindua sauti yake na mtandao wa data katika nchi ya Pembe ya Afrika mwaka jana na imesajili watumiaji zaidi ya milioni mbili.

Safaricom ilianzisha huduma ya M-Pesa nchini Kenya mwaka 2007. Huduma hiyo imekuwa ni biashara kubwa sana kwa kampuni hiyo na pia inatoa huduma kama hizo huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Misri, Ghana, Kenya, Lesotho, Msumbiji na Tanzania.

"M-Pesa inajulikana kufanya mabadiliko ya ushirikishwaji kifedha," alisema Stanley Njoroge, Mkuu Mtendaji wa muda wa Safaricom nchini humo "Tutaendelea kupanua huduma kwa wateja wetu kupitia jukwaa la M-Pesa."

Safaricom ni kampuni ya kwanza binafsi ya mawasiliano nchini Ethiopia, baada ya serikali kulegeza masharti mwaka 2019, sekta ambayo kwa muda mrefu imekuwa inaongozwa na kampuni ya Ethio Telecom inayodhibitiwa na serikali.

Kampuni hiyo ambayo inafanya majaribio Ethiopia, nchi ambayo ina takriban watu milioni 120 ni moja ya nchi yenye idadi kubwa ya vijana barani Afrika, imefanya hivyo wakitabiri ukuaji mkubwa wa huduma hiyo katika miaka ijayo.

Kampuni hiyo pia inakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka katika kampuni ya Ethio Telecom, ambayo faida yake iliongezeka zaidi ya mara mbili katika mwaka wake wa kifedha wa hivi karibuni. Mwezi Julai, Ethiopia Telecom iliripoti kuwa na zaidi ya milioni 34 watu waliojiunga na huduma zake za pesa ya kwa njia ya simu ya Telebirr.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG