Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 16:53

AU imesema inafanya mkutano kuangazia hali ya kisiasa nchini Niger


Rais aliyepinduliwa Niger Mohamed Bazoum
Rais aliyepinduliwa Niger Mohamed Bazoum

Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika linakutana kupokea taarifa juu ya mabadiliko ya hali nchini Niger na juhudi za kushughulikia hilo, chombo hicho cha Afrika kilisema katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa X ambao zamani ulijulikana kama Twitter

Umoja wa Afrika (AU) umesema unafanya mkutano Jumatatu juu ya mgogoro wa Niger kufuatia mapinduzi ya Julai 26 yaliyomng'oa madarakani Rais Mohamed Bazoum.

Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika linakutana kupokea taarifa juu ya mabadiliko ya hali nchini Niger na juhudi za kushughulikia hilo, chombo hicho cha Afrika kilisema katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa X ambao zamani ulijulikana kama Twitter.

Mkutano huo unafanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Waliohudhuria ni pamoja na mkuu wa tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat pamoja na wawakilishi kutoka Niger na jumuiya ya uchumi ya Afrika magharibi (ECOWAS).

Wiki iliyopita, Faki alielezea wasiwasi mkubwa juu ya hali mbaya ya Bazoum amaye yuko kizuizini, akieleza huduma anazopatiwa akiwa mikononi mwa viongozi wa mapinduzi hazikubaliki.

Siku ya Jumapili, utawala wa kijeshi wa Niger uliapa kumfungulia mashtaka Bazoum aliyechaguliwa kidemokrasia kwa uhaini wa hali ya juu na kuishutumu ECOWAS kwa kuiwekea vikwazo nchi hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG