Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 10:52

Ukraine yahamasisha uungwaji mkono wa kimataifa katika mazungumzo ya amani yalioandaliwa na Saudi Arabia


FILE - Picha na Shirika la Habari la Saudi Arabia: Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, katikati, akipokelewa na Prince Badr Bin Sultan, kulia, uwanja wa ndege wa Jeddah, Saudi Arabia, May 19, 2023.
FILE - Picha na Shirika la Habari la Saudi Arabia: Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, katikati, akipokelewa na Prince Badr Bin Sultan, kulia, uwanja wa ndege wa Jeddah, Saudi Arabia, May 19, 2023.

Ukraine na washirika wake wanaandaa kuhamasisha uungaji mkono wa kimataifa kuhusu mpango wa amani utakaojadiliwa wakati wa mazungumzo ambayo Saudi Arabia itakuwa mwenyeji wa mkutano huo mwishoni mwa wiki.

Wanadiplomasia wa Ukraine na nchi za Magharibi wana matumaini kuwa mkutano huo utakaofanyika katika mji wa bandari wa Jeddah nchini Saudi Arabia utakuwa ni fursa kwa maafisa kukubaliana misingi muhimu ya kutambulisha mkataba wowote wa amani ambao utamaliza vita vya Russia vinavyoendelea nchini Ukraine.

Takriban nchi 40 zimepanga kuwakilishwa katika kikao hicho, lakini hivi sasa haiko bayana iwapo China itakuwa kati ya nchi hizo. China ilikaribishwa katika duru za mazungumzo yaliyopita huko Denmark mwezi Juni lakini haikuhudhuria.

Mkutano huo unatarajiwa kuanza siku ya Ijumaa, na majadiliano muhimu yatafanyika siku ya Jumamosi na Jumapili.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema Jumatano ana matumaini mazungumzo ya mwishoni mwa wiki yatapelekea kufanyika “mkutano wa amani” mkubwa zaidi wa viongozi wa dunia wakati wa kuwasili kipindi cha baridi.

Russia haitahusishwa katika mazungumzo ya wikiendi hii au katika mkutano uliopangwa na Zelenskyy utakaofanyika kipindi cha baridi.

Mbali na nchi no za Magharibi zinazo muunga mkono, Ukraine ina matumaini ya kupata uungaji mkono zaidi kidiplomasia kutoka nchi zilizoko kusini duniani, ikiwemo Brazil, India, Afrika Kusini na Uturuki.

Ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Ukraine kupata kuungwa mkono na nchi zilizoko kusini duniani inaripotiwa itasisitiza jinsi bei za vyakula zilivyoongezeka kutokana na Russia kujiondoa katika makubaliano ya mwezi uliopita kuruhusu usafirishaji salama wa nafaka za Ukraine kupitia bahari ya Black Sea na kushambulia ghala za kuhifadhi nafaka katika bandari ya Ukraine.

Kipengele hicho cha mgogoro huo kimekuwa ni fikra ya juu kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, ambaye Alhamisi alizihimiza nchi zote katika Umoja wa Mataifa kuiambia Moscow kuacha kutumia bahari ya Black Sea kuleta madhara baada ya Russia kuua juhudi za usafirishaji nafaka kupitia bahari ya Black Sea.

Baadhi ya taarifa katika habari hii chanzo chake ni mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG