Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 05:55

Blinken kuongoza mkutano wa UN wa ukosefu wa usalama wa chakula


Antony Blinken
Antony Blinken

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ataongoza mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Alhamisi ambao utaangazia ukosefu wa  usalama wa chakula na mizozo  ambayo inafanya hali hiyo iwe mbaya zaidi.

“Tunajua hili kwa uhakika: Palipo na vita, kuna njaa,” Balozi wa Marekani Linda Thomas –Greenfield aliwaambia waandishi katika mkutano wa waandishi wa habari Jumanne akianza nafasi yake urais wa Baraza la Usalama kwa Washington mwezi huu.

Alisema Blinken atakuwa na matangazo kadhaa na vitu vya kuwasilisha” siku ya Alhamisi, na ameyataka mataifa kusaini rasimu ya makubaliano ya mipango ya Washington kwa suala linalohusu maudhui hayo.

Thomas-Greenfield, ambaye amekuwa mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa tangu Februari 2021, alsema atatumia nafasi ya urais wa kupokezana wa baraza hilo kusukuma mbele suala la kutokuwepo usalama wa chakula duniani kuwa ni ajenda ya juu kabisa ya baraza hilo.

Linda Thomas-Greenfield
Linda Thomas-Greenfield

Balozi amesimamia baraza hilo lenye nchi 15 mara mbili hapo kabla kwa niaba ya Marekani, na mara zote alikuwa amejikita katika suala hilo.

Ripoti ya kila mwaka ya usalama wa chakula iliyotolewa mwezi uliopita na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa dunia bado inajikwamua kutoka katika kuzorota kwa uchumi kulikotokana na janga la COVID-19 na pia inaendelea kukabiliana na athari za vita huko Ukraine vinavyoathiri soko la chakula na nishati.

FAO inakadiria kuwa watu milioni 691 hadi 783 duniani walikabiliwa na njaa mwaka 2022, ikiwa kiwango cha juu kabisa kuliko mwaka 2019 kabla ya janga la COVID-19.

Sehemu kubwa ya njaa hiyo ilikuwa katika ngazi ya kanda, ambapo Afrika, Caribbean na Asia Magharibi zikishuhudia kuongezeka kwa viwango vya njaa.

Forum

XS
SM
MD
LG