Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:32

Kerry asema ushirikiano katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa unaweza kuboresha uhusiano wa Marekani na China


Balozi wa Hali ya Hewa wa Marekani John Kerry alipokutana na mwenzake Xie Zhenhua mjini Beijing.
Balozi wa Hali ya Hewa wa Marekani John Kerry alipokutana na mwenzake Xie Zhenhua mjini Beijing.

Balozi wa Hali ya Hewa wa Marekani John Kerry amemwambia mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa China Wang Yi Alhamisi kuwa ana matarajio hatua ya kushughulikia tishio la mabadiliko ya hali ya hewa inaweza kuwa njia ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

“Tuna matumaini sana ya kuwa huu unaweza kuwa ni mwanzo, siyo tu wa mazungumzo kati yako na mimi na sisi kuhusu kushughulikia hali ya hewa, lakini tunaweza kuanza mahusiano mapana zaidi,” Kerry alimwambia Wang alipokuwa anazuru Beijing.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema Kerry amesisitiza haja kwa China “kuongeza kasi ya kupunguza hewa ya sumu, kupunguza uchafuzi unaosababishwa na kemikali ya methane na kudhibiti ukataji miti.

Marekani na China ni wachafuzi wa juu wa gesi chafu za viwandani.

Wang alisema China inaamini kuwa nchi hizo mbili zinaweza “kupata ufumbuzi sahihi wa tatizo lolote” kupitia mazungumzo mapya.

Kerry pia alikutana Jumanne na Waziri Mkuu wa China Li Qiang, aliyesema kuwa Marekani na China ni lazima waimarishe uratibu katika kutatua “changamoto yenye kuhofisha” ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Mazungumzo ya Jumanne yalifuatia mkutano wa Jumatatu kati ya Kerry na mwenzake wa China Xie Zhenhua.

Kerry ni afisa wa Marekani ambaye hivi karibuni amesafiri kwenda Beijing katikati ya msukumo wa kuboresha uhusiano kati ya nchi hizi, kufuatia ziara za Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken na Waziri wa Fedha Janet Yellen.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii imetokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG