Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:16

John Kerry amewasili China kuhusu majadiliano ya hali ya hewa ya nchi mbili


 John Kerry, mjumbe wa Marekani kuhusu masuala ya hali ya hewa. April 16, 2023.
John Kerry, mjumbe wa Marekani kuhusu masuala ya hali ya hewa. April 16, 2023.

Ziara ya Kerry nchini China ambako atakutana na mwenzake Xie Zhenhua, inafuatia wiki kadhaa za rekodi ya joto kali ambapo wanasayansi wanasema joto hilo linazidishwa na mabadiliko ya hali ya hewa

Mjumbe wa Marekani kuhusu masuala ya hali ya hewa John Kerry aliwasili nchini China siku ya Jumapili vyombo vya habari vya serikali vimeripoti, kuanzisha tena mazungumzo yaliyokwama kati ya nchi hizo mbili kubwa duniani zinazotumia gesi zinazochafua mazingira.

Kuanzia Jumatatu, “China na Marekani zitakuwa na majadiliano ya kina” juu ya masuala ya hali ya hewa, kituo cha televisheni cha serikali CCTV kilisema wakati Kerry alipowasili mjini Beijing. Ziara ya Kerry nchini China, ambako atakutana na mwenzake Xie Zhenhua, inafuatia wiki kadhaa za rekodi ya joto kali ambapo wanasayansi wanasema joto hilo linazidishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mazungumzo ya hali ya hewa ya pande mbili yalikwama mwaka jana baada ya Nancy Pelosi, aliyekuwa spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, alipoitembelea Taiwan inayojitawala na kuikasirisha Beijing, ambayo inaona kisiwa hicho kuwa ni eneo lake.

Forum

XS
SM
MD
LG