Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:07
VOA Direct Packages

Mvua za masika zasababisha maafa Korea Kusini


Mafuriko kutokana mvua za masika Korea Kusini
Mafuriko kutokana mvua za masika Korea Kusini

Maafisa wa Korea Kusini wamesema Jumamosi kwamba takriban watu 7 wamekufa kutokana na mvua za masika ambazo zimekuwa zikinyesha nchini humo kwa siku mbili zilizopita.

Wengine 7 wamejeruhiwa na wawili hawajulikani walipo, kulingana na taarifa kutoka wizara ya mambo ya Ndani na Usalama, shirika la habari la AP linaripoti.

Maelfu ya watu wameokolewa kutoka kwenye nyumba zao, wakati shughuli hizo zikitarajiwa kuendelea, huku wataalam wa hali ya hewa wakitabiri mvua zaidi zitaendelea kunyesha.

Treni moja imeripotiwa kuacha njia Ijumaa kutokana na taka taka zilizoingia kwenye njia ya reli kwasababu ya mvua. Hakuna ripoti za majeruhi.

Forum

XS
SM
MD
LG